Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wakuu kwema!
Yaliomkuta Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina hatimaye yamemkuta Dk. Angelina Mabula ametakiwa apeleke ushahidi Bungeni kuhusu Kituo cha Afya Sangabuye wodi moja wanaume, wanawake na watoto.
Hii inaleta maana gani kwa Wabunge hawa waliokutana na hili jambo kutoka kwa Spika, na jinsi ilivyo Dk. Angelina Mabula simuoni akitoa hapa lazima apigwe sauso mapema tu.
=========
SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amemwagiza Mbunge wa Ilemela (CCM), Dk. Angelina Mabula kuwasilisha bungeni kesho ushahidi kuhusu madai ya Kituo cha Afya Sangabuye, Manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza kuwalaza katika wodi moja wanaume, wanawake na watoto.
Akitoa maelekezo hayo jana baada ya kipindi cha maswali na majibu, Spika Tulia alisema: "Jana (juzi) katika majibu ya serikali kulikuwa na hoja ya Kituo cha Afya Manispaa ya Ilemela na nilimwagiza mbunge alete ushahidi kwa namna kanuni zetu zinavyotaka, lakini nilikuwa sijampa tarehe ya kuleta huo ushahidi. Sasa nimpe tarehe ya kuleta itakuwa Agosti 30, 2024."
Soma Pia:
Suala hilo liliibuliwa bungeni juzi baada ya mbunge huyo katika swali la nyongeza kulieleza Bunge kuwa kituo hicho kimetokana na kupandishwa hadhi zahanati iliyokuwapo kuwa kituo cha afya mwaka 1999, lakini hadi sasa kina wodi moja inayotumiwa na wanawake, wanaume na watoto.
Mbunge Angelina pia alihoji lini serikali itakamilisha majengo ya kituo hicho pamoja na kujenga uzio.

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge
- Spika Tulia amburuza Luhaga Mpina Kamati ya Maadili