Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,780
Hodi Hodi Wadau wote wa Mtandao wetu pendwa, mtandao nambari one Tanzania, mtandao usio na mafungamano yoyote, Mtandao wa Jamiiforums! Natumaini kuwa leo mmeamka salama bukheri wa afya njema. Wale wote ambao kwa bahati mbaya hali zao kiafya si nzuri basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wapate nafuu ili angalau wapate fursa ya kuchungulia humu juu ya yale yanayoendelea Bungeni Dodoma. Na kama kuna waliotangulia mbele za haki, basi tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie makazi mema huko.
Wadau, kwa siku ya leo kama Mwenyekiti Pandu Amir Kificho alivyotangaza jana ni kuwa Bunge Maalum litaanza saa 3 kamili asubuhi na kazi itakuwa moja tu ambayo ni KURIDHIA RASIMU YA KANUNI ZA BUNGE MAALUM baada ya kusomwa kwa AZIMIO na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni Prof MAHALU. Kwa leo tutarajie hali ya utulivu kuendelea kutamalaki hasa kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na Kamati ya Mashauriano ambayo kiukweli imefanikiwa kuweka mazingira ya utulivu Bungeni.
Kama Kawaida, natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa wadau wetu mbalimbali waliopo ndani na nje ya nchi. Kwa upekee kama kawaida Mkuu Skype pamoja na Mheshimiwa Simiyu Yetu watakuwa wanatoa ushirikiano uoahitajika. Stay aconnected

UPDATES 1
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni amewasilisha Azimio ka Kuunga mkono Kanuni za Bunge Maalum. Wabunge wengi wameridhia Azimio hilo na sasa Rasimu ya Kanuni imepitishwa na kuwa Kanuni za abunge Maalum
UPDATES 2
Mwenyekiti anatoa tangazo la uchaguzi wa Mwenyekiti wa kudumu. Kwamba uchaguzi utafanyika Kesho saa 10 jioni na kwamba fomu zinapatikana kwenye ofisi za Katibu wa Bunge na wa Baraza la wawakilishi. Kuhusu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mwenÿekiti Kificho anasema kuwa utaratibu wa uchaguzi wa nafasi hiyo utatokana na matokeo ya uchaguzi wa Mwenyekiti.
=====

Just now Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Wamekubaliana kupitisha kanuni isipokuwa vifungu viwili bishani. Vinavyohusu kura ya Wazi au ya Siri.
Hii inaonyesha kuwa wamekubali kazi iendelee wakati kamati ikiendelea kukuna vichwa juu ya vifungu hivyo.
#NASUBIRI UCHAGUZI WA Mwenyekiti wa kudumu.
------------------------------------
Ushirikiano wetu kama taifa umeingia katika historia mpya. Naunga mkono 100%. Mhe. Selasini alikuwa sahihi. - Mhe. Mbowe.
-------------------------------------
Uchaguzi wa Mwenyekiti kufanyika kesho, fomu zitaanza kuchukuliwa leo. Kwa mujibu wa kanuni hazionyeshi kuwa Makamu mwenyekiti atachaguliwa kutoka upande gani (Bara au Zanzibar) kimsingi kama Mwenyekiti atatoka Zanzibar basi makamu wake atatoka Tanganyika. And verse versa. Bunge limeahirishwa hadi kesho saa kumi jioni kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa kudumu.
Katika hali isyokuwa ya kawaida baada ya Mwenyekiti wa BML kuwapa nafasi akina Lipiumba, Mbowe, Mbatia na viongozi wa dini na wote kukubaliana na rasimu ya kanuni ghafla aliamuka Mcj Mtikila na kuhoji kwa nini amekuwa hapewi nafasi ya kuongea "Kwa nini sipewi nafasia kuongea? Mi sina neno la baraka kwa nchi yangu? Kwa nini unawapa nafasi ya kuongea watu mnaokubaliana tu? Ni haki yangu kuongea wala si ombi!
Aliendelea kusema Kificho hamuheshimu Mungu kwani haki ni agizo la Mungu, "kwanini huna heshima wewe?" unataka nikuheshimu wakati wewe huniheshimu? Kweli Mtikila ni kiboko maana pamoja na zomea zomea ya wale wenzetu amekomaa na kudai haki yake Mpaka Kificho akajitetea.