#COVID19 Yaliyojiri JamiiForums Clubhouse kwenye Mjadala wa UVIKO-19, Umechanja au haujachanja? Nini mtazamo wako?

#COVID19 Yaliyojiri JamiiForums Clubhouse kwenye Mjadala wa UVIKO-19, Umechanja au haujachanja? Nini mtazamo wako?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Jamii Forums inakukaribisha kwenye Mjadala wa Ugonjwa wa UVIKO-19 na Waliopata Chanjo

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Clubhouse leo Septemba 2, 2021 kuanzia Saa 11:30 jioni hadi saa 2:00 usiku

Link: UVIKO-19: Mjadala wa waliopata Chanjo - JamiiForums

=====

UPDATES:

=====

=> Dkt. Elisha Osati: Kila siku napokea watu ambao wanataka niwahakikishie wakachanjwe. Sio kwamba hawataki ila wanataka uhakika Tukiendelea kutoa elimu itakuwa jambo zuri. Bahati mbaya hatutoi takwimu lakini tuna wagonjwa wengi katika Wodi zetu

=> Dkt. Aikande Kwayu: Wananchi hawawezi kuona tupo serious wakati kuna mikusanyiko mikubwa Ile imani ya kwamba ugonjwa upo, tukachanje lazima tuoneshe hatari ya ugonjwa na tuoneshe tupo serious kupambana

=> Dkt. Aikande Kwayu: Ni muhimu 'ku-engage' Viongozi wa Dini kwa nguvu sana kuhakikisha chanjo inaongelewa Misikitini au Kanisani Issue ya wasiwasi wa chanjo sio Tanzania tu ni duniani

=> Neema Lugangira: Tunahitaji Wataalamu wetu wa Afya kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa sahihi. Vituo vya Afya vipo ngazi zote

=> Mbaraka Islam: Sisi kama Vyombo vya Habari tuna wajibu mkubwa kusaidia jamii. Hili suala linahusu maisha ya watu Tufike mahala tuchukulie hii kama vita kwasababu watu wanakufa. Bahati mbaya tumeweka mzaha

=> Mbaraka Islam: Wanahabari tuziache Habari zinazopotosha. Tuwatumie Wataalamu na wao wajitokeze mara kwa mara kwa kuandika makala, redio nk Sio lazima Serikali au Wabunge wafanye kazi, Watu wote wajitolee

=> Jeff Msangi: Tanzania ingeweza kujaribu kuondoa misinformation kwa kuondoa vitu mbalimbali Kitu ambacho naona kinasumbua kusaidia watu wengi wapate chanjo ni mixed messages. Takwimu zingeweza kusaidia watu kwenda kuchanja. Bila kupeleka taarifa kwa Umma ni sawa na kazi bure

=> Dkt. Francis Furia: Kumekuwa na mabadiliko kwa sasa hivi. Wizara ina timu ya wataalamu ambao wamekuwa wakiendesha vipindi vya TV na Redio Kuna jitihada imefanyika, changamoto ni kwamba ili tuweze kufanikiwa ni lazima iwe effort ya timu yote sio Wataalamu wa Afya pekee

=> Semkae: Suala la trust kwenye chanjo ni muhimu. Mama akimwambia Binti bado hujazaa chanjo itakuletea madhara, binti hana budi kumuamini Familia na mtu anaposhinda ni jambo la kuzingatia, kama unashinda na watu wasioamini chanjo, hata daktari akisema ni salama hatomuamini

=> Neema Lugangira: Lipo kundi kubwa ambalo halijaamua kama linataka kuchanja au la, tunapaswa ku-focus kwenye kundi hilo Political will ipo kubwa sana, lakini lazima tuunganishe effort zote (Wanasiasa, Viongozi wa Dini, Wasanii nk) tuweze kuongea lugha moja

=> Dr Mabula: Ni kwa muda mrefu takwimu za Maambukizi hazijatolewa na hata ukiuliza Wizarani ni kama kila Mtu anamtupia mwingine mpira Kuna Watu wanataka kupata Chanjo lakini kutokana na ratiba zao za majukumu muda wanaopata nafasi wanakuta hakuna Kituo ambacho kipo wazi

=> Onesmo Ole Ngurumwa: Haifai kulazimisha watu kuchanja kwa sababu suala la afya ni suala binafsi > Lakini suala la COVID-19 ni tofauti kwa kuwa ni suala la kitaifa sio binafsi tena

=> Dkt. Namala: Watu wanaotoa taarifa za uongo wafuatwe na wahojiwe na wanahabari, wanaowapa taarifa pia wafuatwe na kuulizwa > Kisha wanahabari wajibu zile hoja za wote wanaotoa taarifa za uongo. Lakini tukiacha waongee tu, tutawagawa watu

=> Neema Lugangira: Tusiwe na hofu kuhusu chanjo zilizopo kuexpire. Hata Afrika Kusini batch kubwa ya kwanza ya chanjo iliexpire Tupo katika sensitive period ambayo chanjo imetambulika. Kuna kundi kubwa lipo katikati halijafanya maamuzi

=> Dkt. Elisha Osati: Hizi dozi za kwanza zinaweza zisifike malengo zikaexpire. Tuliochanja tukijitokeza zaidi na kuwa Mabalozi watu watachanja Ukimbadilisha mtu mmoja kwenye familia, wengine wanabadilika

=> Onesmo Olengurumwa: Huenda tusifikie lengo la uchanjaji. Mentality ya kwamba Tanzania ni kisiwa na hatuwezi kuathiriwa ni kubwa sana Tulikosea kuamini kama Rais amechanja Watanzania wengine nao watachanja. Hatuna coordinated campaign ya watanzania kuchanjwa

=> Dkt. Francis: Tulikosea kukosa mpango wa namna ya kutoa chanjo kwa kudhani kwamba Rais akichanja basi watanzania watachanjo Lazima tuwe na kampeni ya kitaifa ya kuchanja kama tulivyokufa na kampeni ya kitaifa ya COVID-19

=> Neema Lugangira: Kwenye upotoshaji wa masuala ya COVID19, kundi ambalo limeonekana moja kwa moja ni kundi ambalo hata mimi nimo Wataalamu wa Afya mnayo kazi kuhakikisha hakuna jumbe tofauti kati yenu nyuma wa pazia. Lipo kundi ambao halikubali chanjo

=> Dkt. Francis: Kuwalazimisha watu kupata chanjo ni suala zuri, lakini kwa kuwa tunachanjo chache itakuwa haiwezekani kwa kuwa hazitoshi Ukiona juhudi zilizowahi kuwekwa kwenye vitambulisho vya wajasiriamali unaweza ukaona kuwa inawezekana kuwafikia watu wote

=> Dkt. Elisha Osati: Ni kweli mtu anaweza kuugua baada ya kupata chanjo. Malengo mapana ya chanjo sio tu usipate ugonjwa Lazima watu waelewe ukipata chanjo unaweza kuumwa, ila ugonjwa wako utakuwa very 'mild'

Dkt. Maryam: Ukiniuliza chanjo ipo ni bora, mimi nitasema ni chanjo yoyote ambayo ipo mbele yako kwasababu chnajo hizi zote tulizoletewa ni bora

Kama unapata fursa ya kuchanja ni bora kuitumia kuchanja na sio kusubiri chanjo fulani


Maxence Melo: Huu mjadala wa leo ni wa watu walio chanja, Jamiiforums tutaandaa mjadala wa watu ambao hawajachanjwa pia. Tarehe itatangazwa.
#UVIKO3 #JamiiTalks


post_241100289_572110060587423_8431481559058138371_n.jpg
cover_241075005_557117789041946_8222771922208897631_n.jpg
post_241314682_968531527027852_2583694217743544519_n.jpg
post_241283609_1298427340618814_5808853376840295512_n.jpg
post_241081735_543738400166110_6215325852486614668_n.jpg
post_241130680_263203972317185_8684031548509452130_n.jpg
post_241098550_1012040949563478_8469214819112455325_n.jpg
post_241012042_1015702299255162_3728472149246978966_n.jpg
post_241213817_602904227754119_8214207847030851183_n.jpg
post_240991511_561795978357415_3580446684310437718_n.jpg

+
 
Mjadala ungenoga ungekuwa na pende mbili.

Kwa kuwa chanjo ni hiari na washiriki wakuu wote wamechanja bila shaka utakuwa umekosa mizania.

Hata huko walikoendelea, kuna facts za kisayansi kwanini watu wachanje, na kuna wengine wanasema tusifanye haraka ila tujipe muda kujiridhisha.

Na katika hili sehemu ya mjadala ungekuja na swali, kwanini sehemu za Z'bar wanalazimika kurudia chanjo ya JJ ili wanaotaka kwenda kuhiji ndio wapate vibali?

Kwanini kama content ya chanjo iko sawa, kuna kabaguana kwa chanjo fulani kuwa superior na nyingine kuonekana hazina "ithibati"

Kila la heri wana mjadala
 
Ni chanjo gani hapo nyuma walipewa wanadamu kwa ajili ya kujikinga na homa flani kisha wakachanjwa badae waliambukizwa nao wanaathirika? Kwa mfano chanjo ya polio, chanjo ya uti wa mgogo. Chanjo ya ini
 
Mjadala ungenoga ungekuwa na pende mbili.
Kwa kuwa chanjo ni hiari na washiriki wakuu wote wamechanja bila shaka utakuwa umekosa mizania.

Hata huko walikoendelea, kuna facts za kisayansi kwanini watu wachanje, na kuna wengine wanasema tusifanye haraka ila tujipe muda kujiridhisha.
Na katika hili sehemu ya mjadala ungekuja na swali, kwanini sehemu za Z'bar wanalazimika kurudia chanjo ya JJ ili wanaotaka kwenda kuhiji ndio wapate vibali?
Kwanini kama content ya chanjo iko sawa, kuna kabaguana kwa chanjo fulani kuwa superior na nyingine kuonekana hazina "ithibati"

Kila la heri wana mjadala
Asante kwa Mawazo yako. Ila tu, ni kwamba waongeaji haijalishi wamechanjwa au hawajachanjwa. Kila mtu ana uhuru wa kuongea. Yaani unafunguka mawazo yako. Sio kwamba ili ushiriki lazima uwe umechanja.

Click link hapo juu
 
Kuchanja ni muhimu s
ana. Tupambane gonjwa liishe tusije rithisha hili tatizo kwa vizazi vijavyo
 
Back
Top Bottom