Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe leo Januari 11, 2022. SP Jumanne Malangahe amaliza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Januari 13, 2022

Kina Kibatala wanawamudu vizuri sana
mawakili wa serikali.
 
Au eti hawana ushahidi wowote wa sauti/video ya hiyo mipango ya ugaidi, na bado wanataka kesi iendeleee [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kibatala: Kwanini hamkumkamata Mbowe mwezi agust 2020?

Shahidi: Mambo ya kiforensiki

Kibatala: Unafahamu forensic ya kwanza imefanyika july 2021?

Shahidi: Ndiyo

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu unafahamu kila kitu kinachoongelewa mahakamani kinawekwa kumbukumbu (recorded)!
Sheria ni kama siasa tu.... Wakili wake na wakili wako wanaweza wakawa kitu kimoja kutafutia tumbo shibe... Ndio utajua mambo ya recorded
 
Huyu polisi anayetoa ushahidj mbona kama hajui mambo mengi sana?
Huyu shahidi hajui mambo mengi ya kikazi, ni porojo tu!

Kuna sehemu amekiri kwamba, kumbukumbu ni jambo muhimu kwa askari makini, lakini ameshindwa kukumbuka alipoulizwa ataje hata hoteli mbili za pale Arusha alimokuwa anaishi mtuhumiwa.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Lakini kina Ligwenya wanamjua maana walikuwa nae Ngerengere Jeshini.
Mwaka jana nakumbuka, kuna mtuhumiwa mmoja alisema alimuona Urio akiletwa kituo cha polisi, na aliteswa kama wao.

Sasa leo, imejulikana Urio ni informer. Kumbe kile kipondo alichokuwa anapigwa Urio lilikuwa ni igizo! Du!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kinachoshangaza, aliyewapa information ya mpango wa ugaidi Afande Urio, sio shahidi kwenye hii kesi na mahakama haina maelezo yake...

Huyu Urio angekuwa mtu muhimu sana mahakamani kwenye hii kesi
... watakwambia hawakuona umuhimu wa kumleta mahakamani kama shahidi; kwanini? sijui!
 

Kwa kweli kesi hii inazidi kuliabisha jeshi la Polisi
 
Kibatala Mungu akulinde sana
... that cross-exam ilikuwa balaa kubwa kaka! Anahitaji ulinzi wa jeshi la mbinguni haswa! Maombi maalumu kwa jopo la utetezi; iwe mchana iwe usiku tusiwasahau katika maombi Gabrieli na jeshi lake wakatangulie vita hivi; stadi wa kazi na directives zikitoka moja kwa moja Kiti cha Enzi!
 
Amina
 
Huyu shahidi kajikanyaga mpaka anatia huruma.
... hata ukicheki tone ya wakili wa serikali wakati wa re-exam ni as if "kawaangusha sana huyu kiazi"! Jana Kibatala alipopata nafasi na kuuliza maswali machache kisha kuomba kesi iahirishwe kwa sababu "ana maswali mengi" kwa huyu shahidi nikajua "shughuli ipo"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…