Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 22, 2021. Mahakama yatupilia mbali hoja tatu za utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 23, 2021

Alie elewa msimamo wa jaji atueleza zaidi tafadhari
Soma mwenyewe uelewe. Jaji amechambua sheria vizuri sana kabla ya kuhitimisha hukumu yake. Safi sana. Achana na mambo ya kuja kuambiwa. Ndiyo unavyodanganywa na bush lawyers kwa tafsiri zao za mihemuko ya kisiasa. Soma mwenyewe
 
mimi ikifikia hapa ndio maana nikikamatwa na Polisi kama anataka simu yangu na hela alizonikutanazo hua nampa tu kuepika mengi.

mtu mkubwa kama Mbowe anasoteshwa je mimi ni nani ?🙌
 
Kwani ushahidi wa X KUB kwa upande wa jamhuri umefika mwisho?
bado,
Tunazungumzia mpaka hapa tulipofikia,
nami nime kuuliza kama ulivyo comment, kwamba kwa ushahidi wa shahidi namba 1 hadi namba 8, unaona ukweli na uzito wake vinafanana na ule wa X dc.?
Lakini ..... hautafanana kwa sababu matukio [facts of the case] ni tofauti.
Namanisha ile hali ya ushahidi kutoacha nafasi inayofanya ushahidi huo ulete shaka.

Ushahidi wa X Dc hata kabla ya kufikishwa mahakamani, kwa mtu ambaye aliziona zile video, hawezi ata kuutilia shaka ushahidi ule.

Kwa utofauti huo, huwezi sema ulicho andika hapa down.
Hata X DC wa hai angekuwa CDM mngekuwa mnalalamika hivi hivi.
 
Ah! Tigangaaaaaa. Kweli umeupiga mwingi. Mwenyewe kakiri hamwamini shahidi just a nine day wonder.
 
Uhalali (legacy) wa Serikali ni pale inapokuwepo au kutokana na watu na ipo kwa ajili ya watu

Mkuu wa nchi kupitia chombo cha cha habari maarufu duniani anapo condemn kwa mtuhumiwa ni gaidi/ ana makosa na pia Mkuu wa jeshi la polisi anapothibitisha mbele ya chombo cha habari (Dakika 45 za ITV), huko hakukuwa kuingilia uhuru wa mahakama??
Kama mahakama zetu zingekuwa huru, tungeweza kuamini kwamba Jaji atakuwa huru kutoa hukumu. Lakini kwa mahakama zetu na majaji wetu wanaotegemea kupata vyeo kwa kulamba viatu vya watawala, kamwe haki haiwezi kupatikana au kuonekana ikipatikana.
 
SIKU ZOTE UNAPOELEKEA KWENYE MAFANIKIO NDIO MAUMIVU YANAKUWA MAKUBWA ZAIDI.ILITAKIWA VIONGOZI WA VYAMA PINZANI VYA SIASA WAWE WANAFUNGWA JELA HAPO NDIPO UTAONA UKOMBOZI WAZIWAZI KTK NCHI HII.MM NAONA KUNA MWANGA MBELE.HIVYO SERIKALI IKITAKA TANZANIA MPYA ITENGENEZE KESI NYINGI KAMA ILIVYOTENGENEZA HII YA MBOWE.KUNA SIKU SERIKALI ITAKIONA CHA MTEMA KUNI.
 
Matusi ya nini Brotherman? Kama ulijua ataamua hivi mbona hukumwambia Kibatala aokoe muda wake?
 
Hizi hoja mfu ndizo zinafanya Chadema wanashindwa kwa kila kesi. Mahakama siyo jukwaa la siasa. Acheni kuwahadaa watu na hoja mfu kama hizi kwenye masuala ya kisheria.
Nakushauri kutosoma kwa hisia kali sana vitu vya kawaida na vyepesi. Vinginevyo utakuwa unajidhalilisha kila siku kwa kujianika ulivyo popoma. Wapi nimezungumza CHADEMA? Au una chuki tu binafsi na hicho Chama?. Nilichokisema ni kwamba; Judge ajijikite kwenye Sheria, Kanuni na taratibu katika kutoa maamzi.

Kama unataka kutumianisha kuwa akizingatia hayo, hao unaowaita CHADEMA watashinda basi ndo kilio Cha kila Mtanzania ukiwemo wewe. Tunachokihitaji ni haki si maneno ya nimeamua hivi bila kutaja msingi wa kisheria wa maamzi yenyewe!

Fikiria Askari (Shahidi) hajui hata nani alikuwa zamu siku hiyo, kabla ya yeye kuingia wakati kuna kukabidhiana!!! Anajua tu aliyempokea ambaye logically wameshampanga pia!

Kielelezo hakina hata jina lake, lakini analetewa yeye? Walijuaje yeye anakihiitaji, afu Jaji akija anasema ni sawa tu na wewe 'Matome' unashangilia upuuzi wa namna hiyo! Kweli!!!! Acha hizo bn!
 
mimi ikifikia hapa ndio maana nikikamatwa na Polisi kama anataka simu yangu na hela alizonikutanazo hua nampa tu kuepika mengi.

mtu mkubwa kama Mbowe anasoteshwa je mimi ni nani ?🙌
Dola ni shetani kamili. Ukiitafuta battle utapigwa battle hasa, tena ukiwa mwenyewe kabisa.

Wabongo ni mabingwa tu wa mihemko na ushabiki, hawana msaada wowote.

Kila mmoja atakuwa anakushangilia akiwa nyuma ya keyboard, na utagongwa hasaa.
 
Kwa hoja zako na analysis yako nadhani jukwaa hili si level yako. Nakushauri ni vizuri ukabaki kule kule facebook.
 
Mahakama hii inakubaliana na Upande Wa Utetezi kwamba Naibu Msajili hana Mamlaka ya Kutoa Kielelezo, Mamlaka yake ni Kusimamia pale Kielelezo Kinapokuwa Kwenye Chumba Cha Kielelezo. Kusimamia Utolewaji au Kuharibiwa kwa Kielelezo hicho.
 
Lazima ifike mahali, wananchi tunyanyuke na kusema kuwa huu upuuzi hatuwezi kuuvumilia tena.
Raia wa Sudan jana wamefanya yao mpaka Jeshi likasalimu amri! Kwa hapa, ujasili wa kuzuia jeshi hatunao, matokeo yake figisu figisu za KIPUUZI kama hizi tutafanyiwa sana.
 
mimi ikifikia hapa ndio maana nikikamatwa na Polisi kama anataka simu yangu na hela alizonikutanazo hua nampa tu kuepika mengi.

mtu mkubwa kama Mbowe anasoteshwa je mimi ni nani ?[emoji119]

Wewe ni kamdudu tu.
 
Mzee usihangaike na popoma.
 

Wakati mgumu kwa shahidi upande wa jamhuri na wakili wa serikali
 
Lakini turudi nyuma kidogo, huyu jaji ametolewa Mwanza mahususi kuja kusikiliza hii kesi hivyo analipwa pesa nyingi sana kama posho kwa sababu hiyo.

Hivyo sio rahisi kwamba angeweza kuachia hiyo fursa kwa kukubali zile pingamizi kwani angefanya hivyo ndio ingekuwa mwisho wa hii wanayoita "kesi ya ugaidi' na angewekwa kwenye ndege tayari kurejea Mwanza.

Baada ya kufuatilia Proceedings za hii kesi kwanza sioni ni vipi upande wa mashtaka utakavyoweza kuthibitisha madai yao ya ugaidi.

Pili, huyu jaji akiamua kuwatia hatiani washtakiwa kwa sababu za "hisia tu" kama anavyofanya kwenye hizi pingamizi huku dunia nzima ikitizama sipati picha ya nini kitatokea ila itabidi Judiciary nzima ya Tanzania iwe "Completely Overhauled". Tuendelee kufuatilia.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…