JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mjadala wa leo katika Club House ya Jamiiforums unahoji "Nini kifanyikeili nchi ipate tija stahiki kutokana na misaada inayopata kutoka nchi za nje.
Kujiunga na mjadala huu tafadhali gusa link hii hapa chini
www.clubhouse.com
Mjadala umeanza wazungumzaji wanajitambulisha
BAADHI YA HOJA ZINAZOTOLEWA KATIKA MJADALA
Moses: Taasisi ya Wajibu ilianzishwa na aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovic Uttoh
Tunajikita kwenye kuangalia Matumizi ya Fedha za Umma, Uwajibikaji wa Viongozi pamoja Changamoto zinazojitokeza kwenye ripoti za CAG
Moses: Tunaposema Uwajibikaji tunamaanisha waliopewa wajibu na Wananchi kusimamia Rasilimali wanawajibika kuzisimamia
Rasilimali sio zao bali ni za Watanzania ambao wamewapa dhamana ya kuzisimamia na wanatoa majibu ya Usimamizi huo wanapohitajika kufanya hivyo.
Moses: Serikali ina vyanzo mbalimbali vya Mapato ambavyo husaidia Nchi kujiendesha na kutimiza malengo ya Utekelezaji wa Bajeti iliyowekwa
Misaada (grants) na Mikopo ya ndani na nje ni sehemu ya vyanzo vya Mapato vinavyosaidia kutekeleza Bajeti ya Serikali
Moses: Misaada hutolewa kwasababu tofauti tofauti ikiwemo Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Pia, husaidia kutoa huduma za kukabiliana na Majanga yanayojitokeza kwasababu wakati mwingine Majanga hutokea pasipo kutegemewa. Misaada husaidia katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Moses: Kitu kikubwa ktk Misaada/Mikopo ni Uwazi kwani husaidia Watendaji kuwa na Uoga wa ufujaji wa Rasilimali. Kipindi kilichopita Uwazi haukuwa mkubwa ndio maana Watu wameanza kupongeza kinachoonekana sasa kuhusu Uwazi wa Mkopo wa COVID-19 alivyofanya Rais Samia.
Moses: Uwazi wa Mikopo ni jambo moja lakini Uadilifu wa wanaoifanyia kazi nacho ni kitu kingine. Tulipoanza Sera ya Elimu Bure tulitegemea idadi ya Wanafunzi ingeongezeka lakini sasa hivi suala la Ujenzi wa Madarasa ni jambo linalofanyika katika ufinyu wa muda.
Moses: Uwazi na uhuru wa Wananchi kuhoji nini Serikali inafanya kwa ajili yao uliminywa sana. Sasa hivi tunaona Uwazi umeongezeka na hata Vyombo vya Habari vinaandika mambo mbalimbali. Hata ile hali ufungiaji fungiaji Vyombo vya Habari sasa hivi umetulia tofauti na huko nyuma.
Moses: Nidhamu ni jambo la muhimu katika matumizi ya Kodi ni jambo la msingi ili kupunguza misaada tunayopokea. Awamu ya tano iliongeza kwa kiasi fulani nidhamu ya matumizi na tuliona mahitaji yasiyo na ulazima yakipunguzwa. Tuliendelea kukopa kwa sababu inategemea sana jinsi unavyoelekeza fedha.
Jackson: Kwa kuangalia Bajeti ya Serikali tunaweza kusema 3% ndio tunaita Misaada (Grants) lakini sehemu nyingine inayobaki ni Mikopo ambayo inaweza kuwa ya muda mrefu au mfupi.
Jackson: Tunatambua #COVID19 imeongeza sana uhitaji wa Serikali kuhitaji Fedha kutoka nje ili kupambana na hali ya kiuchumi
Madeni huwa tunayahudumia ambapo kwa kiasi kikubwa huwa tunalipa zile riba za hiyo Mikopo
Jackson: Ili tupate tija ni lazima uwe na Mkakati wa kuliendesha jambo pamoja na Sera. Mpaka sasa Tanzania ipo katika mchakato wa kuboresha Sera ya Ukopaji. Kukosa Sera kunasababisha kutojua kwanini tunakopa, lini tunakopa na kwa lengo la kufanyia nini?
Jackson: Changamoto iliyoonekana kwenye Nchi za Afrika ni kushindwa kuoanisha Mikopo inayokopwa na Ukuaji wa Uchumi. Kuna Mikopo inakopwa kwenda kwenye maeneo ambayo hayazalishi chochote mfano Matumizi ya Kiofisi. Kinachohitaji ni Uwazi wa kiasi kinachokopwa na kitafanya nini
Jackson: Mikopo huchukuliwa kwa lengo la kuendeleza Miradi mikubwa ya Maendeleo. Serikali inatakiwa kuanza Mazungumzo na Nchi jirani ambazo tutazipa huduma ili kuweza kuleta tija na kupata Fedha za kigeni, mfano Mradi wa Treni ya Kisasa ili tusije kujikuta tunatumia wenyewe tu.
Jackson: Mpaka sasa Tanzania haina Sera na Mkakati wa Mikopo ambao umeuhishwa na unatekelezwa. Sera iliyopo imeshapitwa na wakati. Hata CAG alishasema hili kwamba Serikali inahitaji kuwa na Sera inayosema tunakopaje, tunakopa wapi na tunatumia vipi hiyo Mikopo.
Jackson: Ni kweli kwamba sio kila Mkopo unaoupata wewe mkopaji ndio utaweka masharti yanayohitajika. Ni kazi ya Wataalamu wa masuala ya Mikopo kuangalia masharti yanayowekwa na kama tunaweza kuyahimili na kuweza kuishauri Serikali hapo.
Jackson: Nimependa 'spirit' ya kwamba Misaada inatulemaza lakini hatuwezi kuamka siku 1 kusema hatuhitaji Misaada. Nafikiri tuweke Mikakati na kuna Matumizi ya Serikali yanaweza kuepukika. Pia, tuangalie namna ya kuongeza Fedha za Serikali lakini kupunguza gharama za ukusanyaji.
WADAU WANAULIZA MASWALI NA KUCHANGIA HOJA
Mchangiaji1: Kuna maswali ya kujiuliza kuhusu misaada:
Je, hii misaada tunayopewa ni misaada au ni mikopo iliyojificha kwa jina la Misaada?
Je, tunajiuliza Marekani anapata wapi fedha za kutujengea barabara na yeye asipate chochote? Hiyo huruma amepata wapi?
Mchangiaji1: Nashauri tuachane na misaada, ikibidi tubaki na mikopo
Mikopo tunayotakiwa kuchukua ni Mikopo ya Kiteknolojia na Mikopo ya Rasilimali watu. Mikopo ya Fedha haitatufanya kuendelea.
Mchangiaji2: Tujidhatiti katika uzalishaji ili kuepuka mikopo. Mimi siamini kwenye misaada kwa kuwa inakuweka kwenye udhaifu inaonesha kuna mipango ilikosewa awali.
Kujiunga na mjadala huu tafadhali gusa link hii hapa chini
Nini kifanyike ili Nchi ipate tija kutokana na Misaada? - JamiiForums
Wednesday, November 10 at 6:00pm EAT with Sam Gidori.