Yaliyojiri katika Mjadala wa "Je, Demokrasia inakwamisha Maendeleo?" katika Clubhouse Jamiiforums

Yaliyojiri katika Mjadala wa "Je, Demokrasia inakwamisha Maendeleo?" katika Clubhouse Jamiiforums

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
1637854695554.png
Demokrasia imekuwa miongoni mwa nguzo muhimu katika Mataifa mbalimbali. Tanzania ni Nchi ya Kidemokrasia kwa mujibu wa Katiba ambayo Viongozi huapa kuilinda wanapoingia madarakani

Kumekuwa na mjadala wa muda mrefu ukiituhumu Demokrasia kukwamisha Maendeleo huku wengine wakidai kuwa ili maendeleo yatokee kunahitajika utawala wa kiimla. Je, wewe una mtazamo gani kuhusu hili?

Ungana nasi katika Mjadala utakaofanyika muda huu jioni kupitia Clubhouse:

Kujiunga gusa link hii hapa chini:
- Je, Demokrasia inakwamisha Maendeleo? - JamiiForums

UPDATES
Aidan Eyakuze:
Demokrasia inaturuhusu sisi kama binadamu wa nchi fulani kujiuliza maswali 2 ya msingi:
1. Nani atazalisha yale yote tunayohitaji kama binadamu?

2. Nani atalipia uzalishaji huo?

Mdau 1: Maendeleo yapo mengi, kuna maendeleo binafsi, ya jumuiya, ya kitaifa na kidunia. Kuna watu wana 'define' Maendeleo kiafya, kiuchumi nk. Ni jambo pana. Demokrasia ina tafsiri tofauti, kila nchi imetofautiana na nyingine. Jamii inatafsiri vipi demokrasia?

Mdau 2: Vipi mtu akisema maendeleo hayana ulinganifu; yaani Maendeleo ni Maendeleo. Watu wote kuna kiwango fulani cha maendeleo wanahitaji kuwa nayo. Mfano apate chakula bora na sehemu ya kulala. Vipi mtu akisema hayo ndiyo tunapaswa kuyaona kama Maendeleo?

Mdau 3: Demokrasia haikwamishi Maendeleo. Demokrasia inampa mtu haki ya kuamua, kuchagua na kuhoji. Bila kuwa na Demokrasia mtu anaweza kuficha vitu maana hakuna wa kumuuliza. Demokrasia haikwamishi maendeleo, bali watu ndiyo hukwamisha

Mdau 4: Viongozi wetu wamepatikana kwa njia ya Demokrasia. Kwa maana hiyo, haiwezi kukwamisha Maendeleo. Kusema Demokrasia inachelewesha Maendeleo mimi nasema hapana. Demokrasia inaleta chachu kubwa. Mfumo ungekuwa unatumika ipasavyo maendeleo yangekuwa mengi.

Mdau 4: Naamini kwenye Uwazi na Uwajibikaji. Kwa Nchi nyingi za Afrika, shida huanza kwenye Haki ya kuhoji. Demokrasia isingeonekana inakwamisha Maendeleo kama uwajibikaji ungekuwepo.

Mdau 5: Nchi ambayo haina Demokrasia Maendeleo yao lazima yatakuwa hafifu. Lengo la kuwepo Demokrasia na kuruhusu watu waweze kushiriki masuala ya kitaifa na kiuchumi ni kukosoa na kuhoji baadhi ya vitu. Unapomfunga mtu mdomo wa kuhoji, Maendeleo hayatakuwepo.
 
Back
Top Bottom