Nimechoka, naenda kulala Hamna jipya hapa labda mpaka kesho yaani ni ubabaishaji mtupu
Me nalala akikatwa muniamshe wakuu
Akikatwa nijuzeni nichinje kakuku kangu maana nakumbuka mwaka 2008
Nimechoka, naenda kulala…Hamna jipya hapa labda mpaka kesho…yaani ni ubabaishaji mtupu
sasa kama wao wamegawanyika unaconclude vp kashindwa. tusubirie tuone hadi mwisho wa uteuzi ktk ccm ama kwingine.Wadau,
Hii nimeikuta Mwanahalisi Online akiandika nguli wa habari za uchunguzi na ukachero,Ndg Saed Kubenea. Soma mwenyewe hapa chini..............
JINA la Edward Lowassa, mmoja wa wasaka urais kwa udi na uvumba, limeenguliwa katika hatua za awali za kinyanganyiro hicho. Anaandika Saed Kubenea (endelea).
Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na mmoja wa viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma zinasema, jina la mwanasiasa huyo machahari limeondolewa kutokana na shinikizo la baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho.Ni kweli jina la Lowassa limeondolewa katika kinyanganyiro hiki. Baadhi ya wakubwa wamekuja na msimamo na wameapa kutosikia mtu anayeitwa Lowassa akikatiza na kuingia NEC, ameeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.
Vikao vya uteuzi vya chama hicho Kamati ya Maadili, Kamati Kuu (CC) na Halamashauri Kuu tayari vimeanza mjini Dodoma mchana huu. Mkutano wa NEC umepagwa kuanza kesho saa nne asubuhi.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, ikiwa jina la Lowassa limeondolewa katika kainyanganyiro hiki katika hatua za awali, basi ndoto za mwanasiasa huyo kushika madaraka ya juu katika nchi, zitakuwa zimezimwa.
Lowassa amekuwa akihaha kutaka kuwa Rais wa Jamhuri tangu mwaka 1995, ambako alijitosa kugombea nafasi hiyo.
Hata hivyo, jina lake liliondolewa katika hatua ya awali baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kumngangania na kushinikiza kuobdolewa kwa jina lake.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Lowassa hakujitosa katika kinyanganyiro hicho; badala yake alimuunga mkono Kikwete kwa makubaliano ya kufanywa kuwa waziri mkuu na baadaye kuwa rais.
Habari zinasema, kuzimwa kwa ndoto za Lowassa, kunafuatia taarifa kuwa mchakato wa uchujaji majina ya wasaka urais kupitia CCM, kuendeshwa na baadhi ya vigogo kutoka idara ya usalama ambayo imesheheni wabaya wake.
Lowassa, mwanasiasa machachari katika siasa za CCM, ni miongoni mwa makada 38 wa chama hicho waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama chao kugombea wa urais wa Jamhuri.
Inaelezwa kuwa vita ya kisiasa anayopigana Lowassa kwa sasa, siyo tena kati yake na chama chake, bali ni kati yake na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
Mgogoro wa Lowassa na TISS unatokana na ukaribu wa mwanasiasa huyo na aliyewahi kupata kuwa Mkurugenzi mkuu wa idara hiyo, Apson Mwangonda.
Lowassa akiteuliwa kugombea nafasi hiyo, atakuwa amewashinda watu wa usalama waliopo sasa; jambo ambalo haliwezi kukubarika, kimeeleza chanzo kimoja cha taarifa mjini Dodoma.
Anaongeza, ikiwa hivyo, maana yake ni kuwa TISS iliyoko kwenye uongozi wa sasa itakuwa imeonyesha udhaifu mkubwa mbele ya Apson anayeratibu mbinu na mikakati ya Lowassa.
Mkurugenzi wa usalama wa sasa, Othuman Rashid anadaiwa kumuunga mkono Bernard Membe, mmoja wa wasaka urais anayetajwa kuwa chaguo la Kikwete.
Katika hatua nyingine, taarifa zinamnukuu mmoja wa viongozi wa kamati kuu akisema, chombo hicho muhimu katika uteuzi wa wagombea urais, imegawanyika.
Mgawanyiko unatokana na baadhi ya watu kutaka Lowassa asikatwe, huku wengine wakisema, sharti aondolewe, anasema mmoja wa watoa taarifa wa gazeti hili.
eti nani?
Kama Zanzibar ni Nchi Uhalali wa Kugombea Bara Unatoka Wapi??
Akikatwa patam akiachwa patam du hatal!!!
ndugu zangu mwenye taarifa za dodoma nani akuingia tano bora
Ni mtu mwenye uwezo wa kununua Polisi yote, Takukuru yote, NA kamati za chama zote... ni zaidi ya Masai-boy!
Wadau,