Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
HISTORIA FUPI
Mkoa wa Kilimanjaro ulianzishwa rasmi mwaka 1963 kwa Tangazo la serikali Na.450 la mwaka huo ukiwa na wilaya za Kilimanjaro na Pare.
Kabla ya Uhuru Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa ni sehemu ya Jimbo la kaskazini (Nothern Province) lililokuwa linaundwa na wilaya za Arusha na Mbulu, Wakati wilaya ya Pare ilikuwa sehemo ya jimbo la Tanga (Tanga Province).
Wakati nchi yetu inapata Uhuru tarehe 9/12/1961 Mkuu wa jimbo la Kaskazini (Provincial Commissioner) alikuwa Mhe.PC Edward Barongo ambaye aliongoza hadi 1963 na kufuatiwa na Mhe. Peter Kisumo, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkoa wa Kilimanjaro una watu wapatao 1,640,087, ambao ni nguvu kazi muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mkoa huu una eneo la kilomita za mraba 13,209, likiwa na rasilimali nyingi za asili na mazingira mazuri ya kilimo.
SOMA PIA: Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA KILIMANJARO
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.
Chanzo: TAMISEMI
MAMLAKA ZA MIJI
Katika mamlaka za miji, kuna Manispaa ya Moshi ambayo ina kata 21 na vitongoji 60.
MAMLAKA ZA WILAYA
Mkoa wa Kilimanjaro una wilaya sita ambazo zina idadi tofauti ya kata, vijiji, na vitongoji.
1. Wilaya ya Hai ina kata 1, vijiji 62, na vitongoji 292.
2. Wilaya ya Siha haina vijiji wala vitongoji, lakini ina kata 1 na vitongoji 17.
3. Wilaya ya Moshi ina kata 1, vijiji 157, na vitongoji 700.
4. Wilaya ya Mwanga ina kata 1, vijiji 72, na vitongoji 282.
5. Wilaya ya Rombo ikiwa na kata 1, vijiji 68, na vitongoji 312.
6. Wilaya ya Same ina kata 1, vijiji 100, na vitongoji 503.
Kwa ujumla, mkoa wa Kilimanjaro una halmashauri tano, ukijumuisha kata 169, mitaa 60, vijiji 519, na vitongoji 2,258.
MAJIMBO YA KIUCHAGUZI
Mkoa wa Kilimanjaro unajumuisha majimbo tisa (9) ya uchaguzi ambayo yanatoa nafasi kwa wananchi kuchagua wawakilishi wao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: Jimbo la Moshi Mjini, Jimbo la Moshi Vijijini, Jimbo la Hai, Jimbo la Siha, Jimbo la Mwanga, Jimbo la Rombo, Jimbo la Same Mashariki, Jimbo la Same Magharibi, Jimbo la Vunjo
HALI YA KISIASA
Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa ni miongoni mwa mikoa iliyokuwa inashikiliwa na vyama vya upinzani katika majimbo ya uchaguzi mkoani humo ambapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 CHADEMA chini ya mwavuli wa UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) uliohusisha vyama vingine vitatu (3) wakati huo vya CUF, NCCR Mageuzi na NLD, vilishinda majimbo saba 7 kati ya tisa 9 ya mkoa wa Kilimanjaro.
Majimbo yaliyokuwa yakishikiliwa na upinzani ni Same Mashariki, Rombo, Vunjo, Moshi vijijini, Moshi mjini, Hai na Siha, huku CCM ikiambulia majimbo ya Mwanga na Same pekee.
Nguvu hii ya upinzani mkoani humo ilififia kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambapo wagombea kutoka Chama tawala CCM walipita bila kupingwa kutoka na kuenguliwa kwa wagombea wa vyama vya upinzani kwa madai ya kukosa sifa za kugombea hivyo kupelekea baadhi ya vyama kujiondoa katika uchaguzi huo. Kadhalika, uchaguzi mkuu wa 2020 ambao ulipeleka ushindi mkubwa kwa CCM na kuwaondoa wabunge wa upinzani katika mkoa huo.
Katika kujiimarisha kuelekea katika uchaguzi wa serikali za miataa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 vyama vya siasa vimekuwa vikifanya mikutano ya hadhara ili kujiongezea nafasi ya ushindi katika chaguzi hizo.
MATUKIO KUELEKEA NOVEMBA 27
- Rais Samia Kuzindua Rasmi Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa
- Kuelekea 2025 - Rais Samia kuzindua uandikishaji wa Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa Oktoba 11, 2024 - Dodoma
- LIVE - Rais Samia anashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- LGE2024 - Kilimanjaro: Kituo cha kujiandikisha kupiga kura kimewekwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa kitongoji ambaye naye ni mgombea wa CCM
- Freeman Mbowe ajiandikisha Uchaguzi Serikali za Mitaa
- LGE2024 - News Alert: - Waziri Mchengerwa afafanua kuhusu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, leo Oktoba 15, 2024
- Kilimanjaro: Mzozo mkali wazuka kituo Bubu Vunjo, Watu wakiandikishwa kiholela
- LGE2024 - News Alert: - Waziri Mchengerwa: Jumla ya wapiga kura milioni 31, 282,331 wamejiandikisha kupiga kura Uchaguzi Serikali za Mitaa 2024
- Mwenyekiti CHADEMA (Siha - Kilimanjaro) adai kuna Watu 200 wameandikishwa ambao sio wakazi wa kitongoji chake
- Kuelekea 2025 - LGE2024 - Mahakama yaipa Ruhusa TAMISEMI kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Freeman Mbowe: Pambaneni kuhakikisha hakuna kura inapotea
- Kilimanjaro: Mgombea wa CCM akana kumuwekea pingamizi mgombea wa CHADEMA, msimamizi wa uchaguzi anaduwaa
- Wanachama CCM zaidi ya 200 Kata ya Kia wajitokeza kuchukua fomu kugombea Uchaguzi Serikali za Mitaa
- Same: Polisi yazuia mkutano wa hadhara wa Tundu Lissu, yasema ni kufanya kampeni uchaguzi S/mitaa kabla ya muda
- Mchengerwa: Wagombea ambao hawajaridhishwa na uteuzi, waweke pingamizi
- Kilimanjaro: Inadaiwa Polisi wakitumia gari ya Mwenyekiti wa Halmashauri wameenda kubandika orodha wagombea nje ya muda kinyume na sheria
- Polisi: Kuna chama cha Siasa kinapanga kufanya Vurugu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa
- Hai: Wagombea CHADEMA wadai kujaziwa fomu kuwa walemavu
- Moshi: Rufaa zote za CHADEMA zaangukia pua
- Makalla: Chagueni wagombea wa CCM wale wa CHADEMA Mbowe kasema hawana ILANI ni hatari kuwa na kiongozi bila kuwa na Mkataba wa atakufanyia nini
- Same: Wananchi waingia mtaani kwa ajili Mwembe Mbaga Samia Day kuhamasisha ushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- CCM Wilaya ya Hai Yazidi Kuvuna Wanachama wa CHADEMA
- Askofu Shoo: Kampeni zimeanza na upinzani wameanza kunyanyaswa!
- DC Rombo: Uchaguzi utakuwa Huru na wa Haki, 4R zitatumika
- Askofu Shoo afafanua madai ya kuhongwa Tsh. Milioni 150, asema ni mbinu za kumnyamazisha
- Kilimanjaro: Naibu Waziri Ummy Nderiananga apiga kura Kiriche katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Mchengerwa: Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya saa 72
- ACT Wazalendo waelezea rafu walizokutana nazo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Kilimanjaro: Mbowe ashiriki kupiga kura uchaguzi serikali za mitaa