Ile aliyosema kuwa Vijana wengi hawaipendi CCM na wahamia upinzani????
Au ni Ipi maana hii ndio nzito zaidi kama mke wa kiongozi mkuu wa nchi amekiri kuwa Vijana wengi ambao ndio wapiga kura 70% ya nchi wanasupport upinzani iweje REDET na SYNOVATE waseme JK atashinda kwa 80% takwimi gani au kigezo gani walitumia kutupa tathimini hiyo??
Vijana wanachukia CCM-Mama Salma
Na Patrick Mabula, Kahama
MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete amewataka wanawake kuwakalisha chini vijana wao na kuwataka wakipende Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa katika kipindi hiki wengi wao wameonesha kuwa upande wa upinzani.
Akizungumza na wanawake juzi katika ofisi ya CCM ya Wilaya ya Kahama, Mama Kikwete aliwaagiza wanawake katika familia zao kuwakalisha chini vijana na kuwaasa waachane na vyama vya upinzani.
Mama Kikwete ambaye yuko katika kampeni za kumpigia kampeni mume wake, alisema vijana wa sasa hivi kuanzia miaka 18 na kuendelea wameonesha kuwa hawakitaki Chama Cha Mapinduzi kwa vile hawajui mazuri iliyoyafanya na itakayoendelea kuyafanya.
Vijana wa sasa hivi kuanzia miaka 18 na kuendelea sijui wameigiliwa na nini vichwani mwao, huko wanakokwenda hakueleweki, kwa kuwa akinamama tumewazaa naomba huko katika familia zetu tuwakalishe chini tuwaase wabaki CCM, alisema Mama Kikwete.
Mama Kikwete aliwataka wanawake kuacha makundi na kununiana ovyo kwa ajili ya kura za maoni, kwa kuwa zimepita na tumepata wagombea kwa tiketi ya CCM tuache hali hiyo na tuwe kitu kimoja ili kukiletea ushindi chama chetu.
Akiwapigia kampeni wagombea ubunge na udiwani wa majimbo ya Kahama na Msalala, Mama Kikwete aliwataka wanawake kuhakikisha CCM inapata ushindi kuanzia kwenye urais, wabunge hadi madiwani.
Alisema mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala anayetetea nafasi hiyo, Bw. Ezekiel Maige ni kijana makini sana, mwenye busara na katika kipindi alichomaliza ameonekana kufanya kazi zake vizuri hivyo lazima wamuenzi kwa kumpa kura ili aendelee kuwatumikia.
Alisema CCM imefanya mambo mengi mazuri kwa upande wa elimu, afya, miundombinu ya barabara chini ya Rais Kikwete na itaendelea kutekeleza ilani yake, hivyo ni lazima tuhakikishe ushindi wa kishindo kwa wagombea wake kwa kuchagua mafiga matatu-rais, bbunge na diwani kutoka CCM. Source: Majira