Yaliyojiri Mahakama Kuu divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, kesi ya Mbowe na wenzake - 30 Nov 2021

Amejibu vema kabisa , anajua anachokisema, precisely!
 
Sheria ya askari hairuhusu hilo,lazima kuwe na movmne order na task unayofanya mahaki ulipo.in short Nazi ya askari INA mipaka ukiingia kwenye mipaka ya mwingine lazima uwe na movement order,hilo unalosema linawezekana kwa tiss siyo jeshi lingine.Nenda kwenye PGO
 
Wewe ni askari polisi au mwanasheria?
 
Hivi unakuaje mtu mzima kama wewe huna akili??Mbowe sio gaidi
Kwako wewe haki ni kina Mbowe kushinda!!

Ushahidi wa upande wa mashitaka ni wa wazi sana. Mawakili wa utetezi wamepwaya sana. Hivyo tuiache mahakama itende haki.
 
Yule Bashir alitesa sana watu kwa miaka, fukuto la hasira za watu likirundikana kwa miaka, hatimaye liliwashwa na msichana mdogo tu Bashir akang'olewa. Haya yanayoendelea hapa, CCM wanafurahia na kukenua meno wakiringia TISS na Polisi, baadaye, hata kama siyo leo, fukuto la hasira litawaka tu na nchi kuingia matatizoni.
 
Yule Bashir alitesa sana watu kwa miaka, fukuto la hasira za watu likirundikana kwa miaka, hatimaye liliwashwa na msichana mdogo tu Bashir akang'olewa. Haya yanayoendelea hapa, CCM wanafurahia na kukenua meno wakiringia TISS na Polisi, baadaye, hata kama siyo leo, fukuto la hasira litawaka tu na nchi kuingia matatizoni.
 
Naomba unisaidie kuona ushahidi wowote au kielelezo chochote kinachoonyesha 'kula njama kutenda vitendo vya kigaidi'. Najaribu kutafuta kila siku sijafanikiwa. Labda ni mimi sielewi.
Hamna vielelezo vyovyote zaidi ya hayo maelezo ya kulazimisha ya akina Adam.. ukiondoa hayo maelezo hamna kesi hapo. Na sijaelewa mantiki ya wao kudai walichukulia maelezo Central, kwanini toka mwanzo wasingetaja Tazara au Mbweni...
 
Mwendelezo upetoka kweli?
 
Maoni yako yanaonyesha umetumwa ila nakukumbusha tu kuwa iwe oungo ama ukweli mungu anajua kila kitu unaweza kimfunga mtu kwa makosa ambayo hajayatenda kwa kuwa tu wewe umejiandaa namna ya kumshitaki mtu husika ila ki uhalisia yeye sio mkosaji kuna mekosa ya kibinadamu ila kuna dhambi kwa mungu mizani ya haki ipo kwa Allah
 
Lakini lazima awe amejaza form maalum kwenda kufanya kazi nje ya kituo chake Cha kazi hiyo ndiyo kibatala alitaka kuona ili ajiridhishe kuwa alifanya kazi kwa mujibu wa sheria ya kazi yake
 
Hahaaa kwa maslahi ya taifa polisi anaweza kutumika popote
Yaani polisi wa musoma kakutana na jambazi sugu msibani mkuranga,asilishughulikie kisa ni PGO?
 
..kingai,na mahita, walieleza kwamba wao sio askari wa kilimanjaro, bali walikwenda huko kwa kazi maalum...
Hoja dhaifu sana hizo,haziwezi kumuokoa mbowe.

Polisi anaweza kufanya kazi popote.

Mahakama inapochakata ushahidi,inajiegemeza katika kuangalia unamuhusishaje mshitakiwa. Katika kupeleleza polisi wanaweza kumtoa askari nachingwea,kwa sababu ana utaalam na ugaidi ili aende maswa kuna tukio.

Kibatala anatakiwa ajipange kupangua ushadi,sio kupinga mashahidi sijui huyu anatoka kyela kafikaje Arusha,mteja wake atazama
 
Upo sahihi kabisa mwenyewe natafuta uhalisia wa makosa ya kula njama kutenda ugaidi sijaona zaidi naona tu matayarisho ya serikali na mawakili wake kuwapa watu makosa wasio yajua hawa wanaokuja na vi post vyao wametumwa kupima upepo wa wananchi katika hili kujua support yao mtandaoni ila wao wenyewe wanajua ni uongo wanaandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…