Yaliyojiri Uwanja wa Taifa, mpira kati ya Yanga ya Tanzania na APR ya Rwanda, Yanga imesonga mbele

Yaliyojiri Uwanja wa Taifa, mpira kati ya Yanga ya Tanzania na APR ya Rwanda, Yanga imesonga mbele

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
54,762
Reaction score
59,204
Wachezaji wa Yanga watakaoanza ni;

1. Ally Mustapha
2. Mbuyu Twit
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Pato Ngonyani
7. Haruna Niyonzima
8. Thabani Kamusoko
9. Donald Ngoma
10. Amisi Tambwe
11. Deus Kaseke


Wachezaji wa APR watakaoanza ni;
1. Jean Claude Ndoli
2.Rusheshangoga Michael
3.Rutanga Eric
4.Rwatubyaye Abdul
5.Bayisenge Emiry
6.Yannick Mukunzi
7.Fiston Nkinzingabo
8.Benedata Jamvier
9.Bigirimana Issa
10.Iranzi Jean Claude
11.Sibomana Patrick

SUB
Kwizera Olivier
Rwigema Yves
Usengimana Faustin
Nshutinamagara Ismael
Djihad Bizimana
Betrand Iradukunda
Ntamuhanga Tumaini


Dk 2, Twite anakwenda kurusha mpira vizuri kabisa lakini Mukunzi anaugonga na kuwa kona inachongwa na Kaseke lakini Ndoli anadaka vizuri kabisa

GOOOOOOOOO Dk 3, Fiston Nkinzingabo anaunganisha krosi nzuri kabisa ya Rutanga Eric na mpira unajaa wavuni vizuri kabisa kwa ulainiii

KADI Dk 5, Niyomzima analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Rusheshangoga

Dk 7, Sibomana nusura afunge tena baada ya mbeki wa Yanga kujichanganya na Bossou anaonekana kulalama

Dk 8, hadi sasa Yanga hawajafanya la maana, wanaonekana kucheza kwa kubutua na hawajiamini au walioanza bila ya mipango na wanatakiwa kutulia

Dk 9, Tambwe anapoteza nafasi ya kwanza ya Yanga, aliunganisha mpira kabisa wa Twite lakini akashindwa kulenga lango.

Dk 11, Ndoli anaonyesha ujuzi kwa kudaka shuti la Tambwe aliyekuwa katika nafasi nzuri

Dk 14, Yanga wanapata kona, inachongwa na Niyinzoma na Kaseke anauwahi mpira na kumkuta Mwinyi lakini anakuwa si makini katika umaliziaji

Dk 14, mpira safi wa adhabu unachongwa na Bayisenge lakini Barthez anadaka vizuri

Dk 20, mashabiki zaidi ya 25,000 waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa wanaonekana kuwa kimya kabisa kwa kuwa Yanga haijaonyesha soka zuri na APR ndiyo wanaonekana kushambulia zaidiDk 16, Bossou analazimika kutoa mpira na kuwa kona baada ya Benedata Jamvier kuingia vizuri. Iranzi anachonga kona lakini haina madhara kwenye lango la Yanga

Dk 22, Niyonzima anapiga krosi safi kabisa, Kamusoko anagonga kichwa, mpira unagonga mwamba na kurudi uwanjani, Ndoli anaudaka vizuri kabisa

Dk 23 hadi 26, APR wanaonekana kutulia zaidi na kucheza vizuri wakiwapa Yanga wakati mgumu

Dk 30, beki Lutanga wa APR analazimika kumwagusha Ngoma aliyekuwa amemtoka. Faulo ni nje kidogo ya 18
GOOOOOOOO Dk 28 Ngoma anampiga chenga
Rutanga Eric na kupiga shuti kali la chinichini ambalo linamzidi Ndoli na kujaa chini

Dk 31 hadi 36, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja huku APR wengi zaidi wakiwa nyuma kuhakikisha hawafanyi makosa tena

Dk 35, APR wanagongeana vizuri lakini Bossou anatibua hesabu zao na kuutoa mpira. Unakua wa kurushwa, unamkuta Iranzi, anapiga shuti kali kabisa lakini hakulenga lango

Dk 43, Kipa Ndoli anafanya kazi nzuri ya kuuwahi mpira miguuni mwa Tambwe. Kama angechelewa kutoka mapema ingekuwa habari nyingine kabisa

Dk 45, Kakusoko anachonga mpira wa faulo, hatariiiiii, mpira unapita juu kidogo ya lango la APR
Dk 44 hadi 45, APR wengi wanaonekana kurudi nyuma na zaidi wanajilinda kama vile sare kwao inawafaa zaidi

MPIRA NI MAPUMZIKO
SUB Dk 46, APR wanamtoa mfungaji Fiston Nkinzingabo anaingia Jihadi Bizmana
Dk 46, mpira kipindi cha pili umeanza na kama kawaida, unaanza kwa kasi ya taratibu kabisa

KADI Dk 52 Tambwe analambwa kadi ya njano kwa kumzuia kipa wa APR kupiga mpira

Dk 54, Yanga wanagongeana vizuri. Hata hivyo bado ile hali ya timu kutaka bao si kubwa sana na zaidi ni ule mpira wa kugongeana

SUB DK 60 Anaingia Msuva kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima aliyekuwa nahodha wa leo. Anampa Bossou kitambaa cha unahodha

Dk 63 hadi 66, mpira unaendelea kuchezwa katikati ya uwanja. Yanga wanaonekana kama wameridhika pia na sare hiyo

SUB Dk 69 Kaseke aliyeumia, anatolewa akiwa amebebwa kwenye machela na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya

SUB Dk 82,anatoka Benedata Jamvier kwa upande wa APR na nafasi yake inachukuliwa na Betrand Iradukunda

Dk 90, APR wanaendelea kugongeana tena, Iranzi anapiga krosi nzuri lakini MWinyi anauwahi mpira na kumpa Mwinyi anayeokoa na kumpa MWashiuya lakini anafanya bla bla kwa kushindwa kumpa pasi nzuri Ngoma

ZINAONGEZWA DAKIKA 4
Yanga wanapoteza nafasi nyingine ya kufunga bao, Mwinyi akiwa katika nafasi nzuri lakini hakuangalia lango na Mpira unakwishaaaa....!!!

Yanga Afrika 1 - 1 APR

Yanga inasonga kwa kwa Yanga 3 - 2 APR
 
Wakimataifa wamepoteana dakika za mwanzo.. Inabidi watulizane
 
Mpaka sasa ni dakika ya ngapi na matokeo yakoje hapo taifa tafadhali tujuze
Dakika ya 22
Wa kimataifa 0:1 APR
Yanga wamekatwaaaa hawaonekani ila wanajaribu kwenda mbele kufanya mashambulizi
.. Hamisi tambwe wanamlinda hawampi nafasi hata moja..
 
Shabiki wa Yanga mimi, kwa Yanga kukataa mechi isioneshwe kisha mshiko mdogo bila kujali mashabiki tuliopo nje ya Dar nasema wapigwe tu.
 
Shabiki wa Yanga mimi, kwa Yanga kukataa mechi isioneshwe kisha mshiko mdogo bila kujali mashabiki tuliopo nje ya Dar nasema wapigwe tu.
Kaka gemu ikiendelea hivi yanga watakula nyingi.. Ila tusiwaombee mabaya.
 
Back
Top Bottom