Yaliyopita si ndwele?

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,635
Reaction score
4,160
[emoji121]
WAKUU,

INAFAHAMIKA KUWA MIMI NI MTU WA AMANI SANA,
NI MWEMA, MPOLE, MKARIMU NA MSTAARABU.

HUWA SIPENDI SHARI NA YEYOTE,
NA NDIO MAANA SIKU HIZI KITAA WANANIITA
*SENETA WA MTWIZ, _The Peace Maker_*.
-------
SASA KUNA WATU WANATAKA KUITUMIA MISEMO YA WAHENGA VIBAYA KUWAPA HASIRA WENZAO ILI TUHARIBIANE *CV*.

-KUNA MWANA ALINIOMBA NIMKOPESHE HELA,

-KABLA HAJANILIPA AKAOMBA NIMKOPESHE INGINE,

-BAADA YA MUDA FLANI AKAJA TENA KUNIKOPA,

-MWEZI HAUJAPITA KAJA KUNIKOPA DENI LA NNE,

-MWISHO WA WIKI ILIYOPITA KAJA KULIA MACHOZI HADI MAGOTINI NIMKOPESHE HELA INGINE KWANI MKEWE ANAUMWA NA NI MJAMZITO!

******
LEO DADA'AKE NA JAMAA AMBAYE WANAKAA PAMOJA
AMENIPA TAARIFA KUWA JAMAA AMEUZA SHAMBA LAKE 1 LA MKURANGA,
HIVYO AMEPATA HELA ZA KUTOSHA KUNILIPA MADENI YANGU YOTE NA PROJECTS ZAKE ZINGINE ZIKAENDELEA KAMA KAWAIDA,
NA WIKENDI HII AMEENDA ZANZIBAR KUFANYA UTALII WA NDANI!

NIKAAMUA KUMPIGIA MWANA MARA KADHAA BILA MAFANIKIO,
NILIPOMTUMIA MESEJI KUMWELEZA UHALISIA NAMI NIKO VIBAYA SINA HATA BUKU 3.
ETI MWANA KANIJIBU,

" Baba Seneta,
Yaliyopita Si Ndwele,
Tugange ya Mbele."
[emoji124][emoji124][emoji124]
---------------------------------------
[emoji121]
WASH'KAJI,

HUYU MWANA ANA NIA GANI HUYU??!!
 
Braza kachukue vitu vyake home uviuze,hata kama ni kusaidiana sio kihivyo aiseeeh!!!
 
Na wewe mwambie akukopeshe mkewe basi akirudi Zanzibar mwambie yalopita si ndwele.
 
kan umemkopesha jumla sh ngap..??

Yawezekana ukamkopesha mtu sh 500 zaid ya mara 6

ok waiter zungusha [emoji481] [emoji481] [emoji481]
 
Mtu akikunyang'anya shati lako, mwongezee na koti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…