Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
YALIYOPITIKA KIPATA NYUMBA NO. 69 WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Ndugu zangu WanaGerezani
Siku ya Gerezani Day nilikuelezeni kwa muhtasari kuhusu makaratasi yaliyokuwa yakichapwa pale Mtaa wa Kipata No. 69 kwa siri na Ally Sykes na mama yetu Bi. Zainab.
Baba yangu alikuwa anaishi nyumba No. 68 na kaona yote kwa macho yake na shule aliyokuwa akisoma pamoja na Abdul na Ally Sykes na watoto wengine wa Dar es Salaam ya miaka ile ilikuwa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Nyumba hii Mtaa wa Kipata No. 68 ilikuwa ya Sheikh Abdallah Simba Liwali wa Songea ambae alikuwa rafiki mkubwa wa babu yangu, Salum Abdallah.
Sheikh Abdallah Simba ndiye baba yake marehemu Bi. Habiba Simba wa Mtaa wa Somali No. 22.
Mtaa huu sasa ni Mtaa wa Omari Londo.
Nakuongezeeni mambo mengine ambayo sikuyaeleza kwa kuwa muda haukutosha.
Kwanza ni kuwa Mzee Kleist aliishi nyumba ile kuanzia miaka ya 1920 hadi mwaka wa 1942 ndipo alipohama na kuhamia Mtaa wa Stanley na Sikukuu baada ya kustaafu Tanganyika Railways alikofanya kazi pamoja na babu yangu.
Mkabala na nyumba hiyo Kipata No. 69 babu yangu aliishi hapo ingawa alikuwa na nyumba yake Mtaa wa Mbaruku jirani na nyumba ya Aziz Ali baba yake Dossa Aziz.
Babu aliishi hapo hapo hadi mwaka wa 1947 alipohamia Tabora baada ya Loco Shed (Karakana ya Tanganyika Railways) kuhamishiwa Tabora.
Historia hii alinieleza mama yangu Bi Zainabu, mke wa Ally Sykes.
Anasema siku moja adhuhuri, jua lilikuwa kali, Nyerere alifika nyumbani kwake hapo Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Kleist).
Mumewe Ally na Abdul Sykes walikuwa wakimsubiri kwani walikuwa wameagana wakutane hapo.
Nyerere alikuwa amekwenda kwa Msajili wa Vyama kushughulikia tasjila ya TANU.
Alipofika Nyerere alimkaribisha lakini alionekana amechoka taabani na mwenye wasiwasi hana raha.
Nyerere alikaa kwenye kiti akaufunika uso wake kwa mikono yake na akawa kimya kwa muda kiasi.
Nyerere alikuwa na habari mbaya.
Nyerere akawaeleza wenzake kuwa serikali ilikuwa imekataa kusajili chama cha TANU.
Nyerere alieleza kuwa serikali imekataa kuipa TANU usajili kwa sababu chama hakika wanachama wa kutosha wala rejesta ya wanachama.
Baada ya kufahamu kuwa serikali imekataa maombi ya TANU kwa kuwa ati haikuwa na wanachama wa kutosha, Abdul akamwagiza Mzee Said Chamwenyewe aende kwao Rufiji kusajili wanachama.
Hii ndivyo ikawa sababu ya wanachama wa kwanza wa TANU watoke Gerezani na Rufiji.
Nyumba hii No. 69 ina mengi sana katika historia ya kupigania uhuru wa Tangnayika na sisi kama WanaGerezani tuna wajibu mkubwa wa kuwasomesha wale ambao hawajui historia ya kuundwa kwa TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
TANU ilipata tasjila yake tarehe 30 Novemba, 1954 baada ya kuzishinda hila nyingi na vizingiti vilivyowekwa na serikali za kupinga usajili wake.