LGE2024 Yaliyotokea chaguzi za 2019 na 2020 ndiyo yanayotokea sasa na kuwakatisha tamaa watu kujiandikisha

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Mtindo unafanywa sasa wa kuwaandikisha watoto wa shule waliochini ya miaka 18 ni dhahiri ni njama za kuhujumu uchaguzi wa serikali za mitaa kwa manufaa ya chama tawala.

Hakuna chama cha upinzani kinachoweza kwenda kuchukua watoto wa shule waliochini ya miaka 18 kwenda kujiandikisha. Haya sasa yanafanyika kwa uwazi na hakuna siri tena kwakuwa tunaona picha za watoto wadogo wanaopelekwa vituoni kujiandikisha.

Nguvu kubwa inayotumika kuwahimiza wananchi haina maana youote kwakuwa tayari zoezi zima limevurugwa na watawala hivyo wananchi wanaojitambua wameshakata tamaa ya kujiandikisha kwakuwa yaliyotokea 2019 ndiyo yanakwenda kutokea 2024.

Soma Pia: Godbless Lema, mlishatwambia kuwa kushiriki chaguzi kwa sheria hizi za sasa ni Ujinga

Kwa ufupi chini ya katiba ya sasa hakutawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki hadi Yesu arudi. Refa anagombea na ndiye anasimamia uchaguzi, anateua tume, ana vyombo vya mabavu, yeye ndiye mwenye uwezo wa kutangaza mshindi anayemtaka yeye na si wapiga kura kama ilivyokuwa 2019 na 2020.

Sasa kuna haja gani ya kuingia mchezoni katika mazingira haya? Kuna haja gani ya kujiandikisha? Kuna haja gani ya kwenda kupiga kura?
 
Mtindo unafanywa sasa wa kuwaandikisha watoto wa shule waliochini ya miaka 18 ni dhahiri ni njama za kuhujumu uchaguzi wa serikali za mitaa kwa manufaa ya chama tawala...
Wale ambao walikuwa hawajui , Hizi ndio zile 4R zinazotajwa kila kona
 
Kwani huko kwenye vituo vya kujiandikisha hakuna mawakala?? Hizi taharuki mnazoeneza huku mitandaoni hazina maana yoyote .. Na mtu yoyote anayehamasisha watu kutojiandikisha kwangu mimi huyo ni adui wa demokrasia..
 
Mtindo unafanywa sasa wa kuwaandikisha watoto wa shule waliochini ya miaka 18 ni dhahiri ni njama za kuhujumu uchaguzi wa serikali za mitaa kwa manufaa ya chama tawala.

Hakuna chama cha upinzani kinachoweza kwenda kuchukua watoto wa shule waliochini ya miaka 18 kwenda kujiandikisha. Haya sasa yanafanyika kwa uwazi na hakuna siri tena kwakuwa tunaona picha za watoto wadogo wanaopelekwa vituoni kujiandikisha.

Nguvu kubwa inayotumika kuwahimiza wananchi haina maana youote kwakuwa tayari zoezi zima limevurugwa na watawala hivyo wananchi wanaojitambua wameshakata tamaa ya kujiandikisha kwakuwa yaliyotokea 2019 ndiyo yanakwenda kutokea 2024.

Soma Pia: Godbless Lema, mlishatwambia kuwa kushiriki chaguzi kwa sheria hizi za sasa ni Ujinga

Kwa ufupi chini ya katiba ya sasa hakutawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki hadi Yesu arudi. Refa anagombea na ndiye anasimamia uchaguzi, anateua tume, ana vyombo vya mabavu, yeye ndiye mwenye uwezo wa kutangaza mshindi anayemtaka yeye na si wapiga kura kama ilivyokuwa 2019 na 2020.

Sasa kuna haja gani ya kuingia mchezoni katika mazingira haya? Kuna haja gani ya kujiandikisha? Kuna haja gani ya kwenda kupiga kura?
Adui wetu mkubwa ni CCM.
 
Back
Top Bottom