Complicator
JF-Expert Member
- Aug 23, 2013
- 2,198
- 3,580
Miguu michafu ya kina lukaku na sanchez, Miguu Iliyobeba nyayo zenye vumbi la dhambi. Ilipothubutu tu kuikanyaga ardhi takatifu ya Mtakatifu James. Ardhi ikapiga kelele ishara ya kwamba kuna watu wamekuja kuitia najisi mji huo mtakatifu, Ndipo gavana katili wa mji wa Newcastle akawauliza diame na Ritchie Mnataka nimfanyeje MANURE?!! Zikasikika kelele ASULUBIWE! ASULUBIWE!
Basi gavana akaamuru MANURE atendewe kama watu wa mji wa NEWCASTLE watakavyo.
NEWCASTLE wakamtwaa MANURE, wakamfanyia dhihaka kwa kumvika nepi kichwani, kisha wakamnyoa ndevu kwa vijinga vya moto.
Wakamtundika kwenye mbao zilizotengezwa mfano wa msalaba. Kisha wakampigilia msumari mkubwa mmoja tu. Mikononi na miguuni. Juu ya kichwa chake wakaweka kibao chenye maneno ya kiitaliano.. Mosi serta hora inserta. Yaani, HUYU NDIYE BINGWA WA UROPA LEAGUE
Baadhi ya askari wasiojua tafsiri ya neno utu tangu wazaliwe. Wakamuona Ed Woodward amejificha akishuhudia mateso ya Manure Wakamfuata nakumuuliza. Wewe nawe u sehemu ya watu hawa?!! Ed akaikana Manure mara 3 kwa kusema maneno haya..
SIJAWAJUA WATU HAO TANGU KUZALIWA KWANGU.'' Baada ya hapo akatoka mbio mithili ya kibaka aliyeichoropoa shingo yake kwenye tairi la moto.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]