Sina nia ya kukebehi imani au dini ya mtu. Lakini lazima itakuwa tumerogwa. Nani AMETUROGA?
Hizi imani vipi? Yaliyotokea Kenya, yanatafakarisha. Pastor Mackenzie na Pastor Odero wamewashawishi wafuasi wao wafunge bila kula ili eti wakifa wakutane na Yesu Kristo. Waumini masikini wakaitikia Naam! Mamia wamekufa. Msitu wa Shakahola umejaa maiti. Kila kukicha wanaokota maiti.
Miaka michache iliyopita nchini Uganda tuliona ya Kibwetere? Waumini takribani mia tisa walidanganywa. Wakajazwa kanisani na kuchomwa moto. Wakafa kijinga kabisa, eti ni safari ya kumuona Yesu Mwokozi.
Tumekuwa tukishuhudia visa na mikasa ya wachungaji na makanisa. Wapo wanaowalisha waumini wao kila takataka (nyoka, mijusi n.k) na wengine kuwanywesha jiki eti ni njia ya kuwatakasa dhidi ya dhambi.
Wapo Wachungaji ambao wakiwa wanaingia Kanisani, waumini hulala kifudifudi ili Mchungaji apite juu ya migongo yao akiwa anaenda madhabahuni.
Wengine (wanawake) wanaambiwa waje na nguo za ndani (chupi) eti ili ziombewe na matatizo yao yataondoka.
Hapa kwetu tunaona wapo wanaouziwa maji yaliyoombewa, chupa ya lita moja Kwa shilingi elfu tano. Maelfu ya katoni za maji yanauzwa na kununuliwa na waumini wajinga na masikini. Nimeshuhudia watu wakiuziwa leso kwa shilingi elfu 5, leso ambayo ukienda dukani ni shilingi mia tano tu.
Wapo wajinga wengine ambao, waliandamana na kuweka kambi airport eti wana wito wa kwenda Jerusalem. Upuuzi.
Wachungaji hawaishi vituko na vibweka kama vya kaboka mchizi. Rafiki yangu mmoja aligombana na mke wake, kisa mke anataka salary slip ya mumewe ili ampelekee Mchungaji akapigiwe percent ya kuwasilisha kanisani kila mwisho wa mwezi.
Miezi michache iliyopita, tulisoma katika magazeti Bwana mmoja ameenda mahakamani kuomba mahakama ikubali kuvunja ndoa ya mume na mke, kisa mke ambaye ni mwalimu ameomba mkopo Benki na mkopo wote kumpa "baba Mchungaji".
NANI AMETUROGA?