- Thread starter
-
- #41
Hilo ni tukio la ngapi? Mumewe kajiteteaje? Yeye bado anaipenda hiyo ndoa? Ukiacha hizo message kuna dalili nyingine mbaya ambazo mumwe kazionyesha kwa Mkewe? Huyo rafiki yako mpaka sasa kachukua hatua gani? Mumewe kaonyesha kujutia au amekomaa? Nijibu kwanza haya maswali
Kwa mujibu wa jirani yangu hii ni mara ya kwanza kuziona sms hizo hii ni kutokana na kutokuwa na mazoea ya kusoma sms kwenye simu ya mumewe. Ila sms zinaonyesha walianza mahusiano muda mrefu. Jirani kaamua kutafuta nyumba apange sehemu nyingine kwani anasema hana imani naye tena. Anadai hivi karibuni mumewe amekuwa akinuna mara kwa mara na kumkaripia hata kwa kosa dogo analolifanya tofauti na mwanzo. Mumewe anadai walikuwa tu wanachati na huyo dada sio mpenzi wake.