Yamenikuta leo Mama G

Mama Sabrina

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
16,620
Reaction score
27,589
Sina hamu na kila kitu hapa ,,ni hivi nilikuwa nafanya usafi chumbani kwangu na kupanga kila kitu ila kuondoa vumbi nimemaliza nikawa nafanya usafi nyumba yote sasa hapo nawaza nikaangalie movie (mission impossible fallout)

nikamaliza kila kitu kikawa mahala pale,kuja kuangalia muda nikawa nimechelewa hiyo movie nikaona kuna muda mwingine ambayo ni saa 1 jioni hii nikasema fresh haina shida ntaenda muda huo ,G wangu akapiga simu tukaanza kuongea weeee tukajipa break maana yupo kazini, si nikasema niende kuoga nimeingia hivi nikaubamiza mlango nikaendelea kuoga ...

Kasheshe likaanza nataka nifungue mlango mamamaweee mlango haufunguki ,vuta vuta wapiiii nikaanza kuuvuta kwa chini hakuna ,,nikashika kitasa nikavuta wapii, nikaona nitoe taulo nitupe pembeni nikaona linanibana ,nimehangaika nyie niko peke yangu nyumba nzima mlango wa sebuleni nimeufunga kwa ndani,,nikawaza sasa hapa hata nikichungulia kwenye dirisha la bafuni nikaita mtu atapitaje wakati sebuleni kule nimefunga mlango ,nikakaa kwenye sinki nimekaa machozi kama yanataka kunitoka maana nimefanya vyote havijanisaidia ,,nikawaza jamani nani sasa atanisaidia simu zipo chumbani tena nimeacha zinalia muziki wa baila ,jamani nikainuka tena nikaanza kuvuta kitasa (nikaanza kupatia picha kama kwenye movie mtu akibomoa mlango)nikapiga teke wapii kumbuka hapo nipo uchi huku narusha mateke kuupiga mlango lakin holaaa.

Nikajisemea alieniambia nije kuoga nanii jamani au uchawi huu,,kumbuka hapo nishaubamiza mlango kwa mateke na kuusukuma kwa nguvu ,kuvuta kitasa kikang'oka nikasema leo ni leo !!!!!!!![emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22] hiii nikaweka taulo chini nikalikalia kabisa nikaanza kuwafikiria watu ninaowajua wangekuwa karibu wangenisaidia ,nimepata tabu leo ,

Nikasema sasa hapa nimeng'oa kitasa nafanyaje sasa nikanyanyuka tena piga teke ,sukuma ,bamiza mpaka mwili ukatoa jasho baadae nikaona nichukue kile kitasa pale pa kushikia nikapageuza ili nianze kung'oa kiubao kilikuwa kimeshikiwa pale kwenye eneo la kitasa bahati nzuri nikaweza kuving'oa baadhi nikaanza kuchokonoa mlango ukafunguka nikapumuua kwa nguvuu nikajimwagia maji halaf nikatoka ,sina hamu nako kabisa nimejilaza hapa nasubiria ifike saa 12 na nusu niondoke zangu nikazurure mall.Hapa mwili unanitetemeka ,vidole vimekosa nguvu ,miguu imechoka yaan nimefanya zoezi kwa lazima..

Basi bana ndio tabu ilonikuta muda si mrefu jamani hebu patia picha usingefunguka ingekuwaje G yupo mbali ningefanyaje majirani wasingenisikia kabisa labda wapita njia ambao siwafahamu

Jioni njema
 
Last edited by a moderator:
Dah pole mama Sabrina!! Nina mkasa unaofanana na wako kidogo,kuna siku panya walikua wanasumbua sana kwenye store ya kihifadhia pumba ya kulisha nguruwe!! Siku moja niko free nikasema ngoja niwakomeshe maana nilikua hata nikiwawekea sumu hawali,.
Nikatoa magunia yote ya pumba nikacha moja tu ambalo kwa chini nilikua na mbao ambazo wamejificha humo.
Nikachukua mpini wa jembe nikawasha na taa yenye mwanga mkali nikabamiza mlango paaaah! Ili nikitembeza rungu wasitoke!! Niuwe wote
Nikatoa lile gunia ambalo kwa chini panya wengi wamejificha kwenye zile mbao,walitoka panya wengi wakirandaranda wasione pakutokea!.
Mi nikaanza kutembeza rungu nikaua wote pamoja na vitoto(sikumbuki idadi)
Nakuja kufungua mlango niwatoe nifanye usafi mlango haufunguki!! Vuta wapi kitasa kimejiloku afu home nipo alone simu ipo chaji geto
Nakumbuka nilikaa mle store kuanzia sasa 11 jioni mpaka kesho yake saa 2 asubuhi ambapo nilipata wazo la kutoboa ceiling board nikapita daarini mpaka kutobozea kwenye korido ya geto
 
Dah....mzee baba pole.....
 
Hahahaha pole sana mkuu
 
Nilichogundua ni kwamba kwanza ulisafiri .. Una nyumba..unapenda muvi za mapigano ...hauna time table specific unafanya fanya vitu kichwa chako kitakavyokutuma .... Unapenda kumsumbua mpenzi wako akiwa kazin kutafuta kipato... Una mlango wa chuma ... Taulo lako jeupe na linakubana bana sana una sinki mama ... Unapenda mziki wa baila .... Lakini kubwa kuliko yote [emoji24] huon aibu kukaa uchi
 
Ahhaahhaahah uwiii ,,,mpenzi wangu simsumbui ye ndio hunipigoa mara nyingi kuzidi hata mimi,uzuri hajaajiriwa so tunaongea muda wowote akitaka na wala sio usumbufu kwake,,,
Napenda movie za mapigano
taulo nimkubwa ila tu nilichanganyikiwa nikaona linanibana.
Baila naupenda mnoo
Sasa bafuni utakaaje na nguo jamani
 
Ulikua ushaoga
 
akikujibu nitag
 
Bora umetoka salama maana sipati picha mlango umejifunga hivyo afu humo bafuni akatokea mjusi,mende au panya nadhani leo usingeweza kuandika hapa
 
Hahahahahahaha pole sana nacheka kama mazuri,,nilichukua ile mop ya kudekia nikaangalia hapo juu kwenye dari nikajisemea naweza kutana na nyoka hukp au nikaumwa na nge bure ,,umenichekesha kumbe we mwenzangu ulikaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…