YAMENIKUTA

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412

Mwaka 1993, Ndugu wawili wa familia moja, Richard Makalla (Easy Dope) na Robert Makalla (D Chief) wanaazisha kundi la muziki wa Rap huko Temeke.

Kundi hilo linatoa burudani ya muziki kupitia matamasha mbalimbali na kujipatia umaarufu mkubwa, hivyo kutoa ushawish kwa vijana wengi wa Temeke kujiingiza kwenye muziki wa Rap.

Mnamo mwaka 1995, vijana hao wawili (Easy Dope na D Chief) wanamuongeza kundini kijana mwingine mkali kutoka Temeke, Rashid Ziada, maarufu kama KR kama anavyojulikana na wengi.

Nawazungumzia "Gangsters With Matatizo" (GWM) hapa, kundi kongwe kabisa la muziki wa Rap nchini, ililochagiza kuibuka kwa vipaji vingi vya muziki huo kutoka wilayani Temeke na kwingineko.

GWM wakaishika bongo, na kuwa tishio haswa katika makundi ya muziki huo yaliyoanza kuibuka na kushika kasi kupitia matamasha ya muziki ambayo yalikuwa platform ya vijana kudhihirisha ubora wa vipaji enzi hizo.

Wakati GWM wakitamba kama kundi, Rapa 2 Proud, baadae Mr 2, kisha sasa Sugu, alikuwa kwenye ubora wake usiopimika kwa upande wa wasanii wanaoimba binafsi bila kundi (Solo Artist)

Katika ubora wao, 1997, GWM na SUGU wakafanya track ya pamoja iitwayo "Yamenikuta" chini ya Prodyuza Bonnie Luv kupitia Studio za Don Bosco. "Yamenikuta" ikawa 'homa ya jiji'.

Wimbo ukadatisha kila mtu. Kuanzia watu wazima mpaka watoto, hakuna ambaye hakuiimba "Yamenikuta" walau kwa mstari mmoja tu wa maneno ayajuayo kwenye wimbo huo.

YAMENIKUTA
-----------------------

Yamenikutaaa..
Yamenikuta,
Yamenikuta,
Yamenikuta,
Mzee mwenzangu.!

Verse 1
------------
Emetufatao-tao
Bili ya mtandao
Lazima, tabia zao-zao
Kikukacho
Kinguoni mwako
Ndugu yako
Aweza kuwa adui
Kama chui, humjui-jui
Mkali kama chui-chui

Ndpo atakapozibia
Bania, Nunia
Zikiisha anakuzushia
Dizaini Iie, Namna ile
Kafumaniwa, Kavamiwa
Na dege lisiloliwa
Kakanyaga miwaya
Anagwaya-gwaya gwaya
Hana lakufanya-fanya

Walimwengu nuksi Duh.!
Watakufuata-fuata fuata
(Wakufuate)
Watakusema-sema sema
(Wakuseme)

Akili ni nywele-nywele
Kila mtu ana zake-zake
Kivyake-vyake
Kimpango wake-wake

Duniani kuna washenzi
Tena wengi, Banyamulenge
Vitiko, Vidigu, Wanyalukolo
Kila kukicha, Kwa visa visa
Kila kukicha, Kwa visa visa

Yamenikuta..
Yamenikuta..
Yamenikuta
Mzee mwenzangu

Sugu verse
-------------------

Yamenikuta.
Mzee mwenzangu
Sina changu
Nabaki na machungu
Wanga wengi anga zangu
Ama zao, Ama zangu
Kiama chao, ama changu

Ukiishi kwa Upanga
Na utakufa kwa Upanga
Mungu ndiye anapanga
Kila kitu, kwa kila mtu
Yamenikuta
Mpaka najuta kuzaliwa

Kheri nife
Kwanini nisife
Maisha haya
Dunia siyo mbaya
Walimwengu ndio wabaya

Kujulikana kuna mambo
Watakusema-sema
Kila Jambo
Hawakawii
Fulani ana H.I.V.
Wanapakaza hivi hivi

Tukirudi kwenye mitaa
Ndiyo balaa, hakuna raha
Polisi wanatughasi
Utasema wana kisasi na sisi
Wanatamani
Watumalize kwa risasi

Kucheka nataka
Kulia nataka
Nabaki mdomo wazi
Wasomi wamejazana
Hakuna kazi

Kilichobaki tukazane tu
Mabibi na mabwana
Kwani hatuna namna Tena

Yamenikuta..
Yamenikuta..
Yamenikuta..
Na wengi yanawakuta
Yaliyonikuta.

Verse 3
------------
Yamenikuta
Mpaka najuta
Valia bukta
Kibwebe
Kwa mambo
Kedekede
Lakini kwa sasa
Ni mpweke

Sijui nicheke
Lakini nashindwa
Maisha ni ubingwa
Na Mambo yamenitinga
Nginga-nginga

Maisha ni kama
Nakwemda- nakwemda
Naweka mpira ule Kati
Nataka kuvagaa
Navutwa shati

Ah piga chenga 1,2,3,
Ah jaza krosi
Lakini kwa sasa
Bongo jua la utosi
Apendwi mtu
Linapendwa pochi

Haa..haaa.. acha-acha
Kupepera mzaha
Navurugu-vurugu mechi
Mbona hueleweki
Kulaaleki
Kufa hakuna breki

Wewe usilete
Ngendembwe
Twakuona
Kilembwe X2

Bora nipate njiti
Nikawe fiti
Na mapande ya mihogo
Usicheze mbali
Na Unga robo

Moja ngoja
Moja Mbili

Nasema na hili
Nakupa na hili
Nashuka shairi
Kwa kiswahili

Nauli yenyewe 150
Bora nishuke chini
Kwa mama ntilie
Anijazie
Nifanye kweli
Eeh bwana
Kiungwana

Toba.!
Sijui nijifanye
Ombaomba
Mgogo
Nipate kitu kidogo
Nishai

Bora nizuke viwanja
Nipate mkwanja
Bongo jua Kali
Na hapo ndipo
Utapotafakari
Maharage ni
Mboga au futari

#Balozi........✍️
 

Attachments

  • 1738145746346.jpg
    133.8 KB · Views: 6
 

Attachments

Mkuu imekaa poa sana inanipa nostalgic feelings mimi kijana wa Gen Z mambo enzi zenu yalikuwa moto sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…