Yamenikutaaa ndugu zangu

Hamjui mnachotaka ktk mahusiano.

Kama ni mapenzi kuweni makini ongeeni kama watu wazima,je umewahi kuongea naye serious?
 
Hiyo window ina virus piga chin weka nyingine.wako wengi ni pm nikupe namba ya dem mmoja anaadabu.
 
Mwanamume kama rijali,unajiamini na unapiga game vizuri hukosi penalti kwa nini ulie lie demu anaposema muachane?achana naye labda kama una weakness zingine.
 
soma alama za nyakati mapema.iyo ni viashiria vibaya sana kama mtakuja anza maisha ya ndoa..pole pambana mwanaume mpaka akuelewe jinsi unavokereka...kama hakusomi piga chini.
 
Sasa mkuu neno tuachane na ndoa tayari vinakinzana. Au sjui Kiswahili sahihi?
 
Mkuu wewe ndo wa kufanya maamuzi magumu! Binafsi nilishawahi kuwa na msichana wa type hiyo. Mkikosona japo kwa jambo dogo, alikuwa anatukana sana kupitia message. Lakini akikaa hasira zikiisha anakuja kuniomba msamaha yanaisha.
Nilijitahidi sana kumuelimisha maana ya safari kimaisha, lakini hakunielewa. Tulifanya mchezo wa kuachana na kurudishiana mara tatu. Nikaja kugundua kumbe alikuwa na uhusiano na mwanaume mmoja mtu mzima ofcn kwao. Japo kazi mi ndo nilimtafutia.
Baada ya hayo nilifanya uamuzi wa kuachana nae, japo alinitukana sana....alifikia hatua hadi ya kuniambia ninaliwa TIGo.
Baada ya miezi mitatu akaanza kunisumbua tena, ati kajifunza kwamba nilikuwa nampenda kweli! Anaomba nimpe chance ya mwisho ( ya nne). Mara ooh we ndo mwanaume ninaekupenda pekee.
Nilihitimisha zoezi kwa shida sana, hadi alipokuja kugundua nimepata mwanamke mwingine.
Ndugu yangu nakushauri achana na huyo mwanamke. Muombe Mungu akupe mwingine, wapo walio tulia kwa aliyetulia pia. All the best!!!!!
 
Kabla ya kuchangia naomba kufahamu
1. Je yeye ni tegemezi kwako?
2. Umewahi kusikia tetesi kama amewahi kua na bwana hapo katikati 2007-date
3. Kabila lake?
4. Umri wake?
Unajua mabinti wengine mnawaweka mjini sana ndo maana wanakua na viburi, lakini kama mmebalance utegemezi wenu its okey

Roughly hakufai, kama hizo kero ni mkabla ya ndoa je utafurahia ndoa yako kweli kwa staili hiyo ya maisha?
 
Huyo dada ananipenda kufa wivu umemzidi mkuu mpaka inakera sana
<br />
<br />
jambo gani linakuonyesha kuwa unapendwa sana,na yote hayo ni wivu 2?kama wewe mkristo soma 1 corinthians 13,utajua upendo ni nini na kama wivu ni upendo,
 
kaka mambo ya mausioano yana mambo mengi sana,ninachoweza kusema kaa chini tafakari, kwetu sisi wakiristo, tunasema marriage is not a word, is a sentence to life, na ndo maana inaitwa pingu za maisha, unaweza kumuoa mambo yakawa magumu sana baadae au mazuri lakini inahitaji ufanye uchunguzi wa kina, ujue kwa nini anasema hivo, kaa na marafki zake, chunguza familia yao, tabia zake kwa ujumla, kama mlikuwa mnakaa vizuri iweje abadilike sasa hivi? kuna mengi sana ambayo yanahitaji moyo wa ujasiri na muda wa kutosha kufanya maamuzi yanayohusu maisha yako yote yaliyobaki hapa duniani!

yangu ni hayo!!!!!!!!
 
Ndugu yangu usisubili inyeshe wakati mawingu unayaona, jitoe katika hayo mausiano, upendo amishia kwa wazazi wako mana wao ndio wanajua thamani yako
 
Vumilia ndugu,ndo mambo ya mahaba yalivyo.
 
huyo mwanamke atakutesa saaaaaaana ndani ya ndoa chukua hatua mapema dalili ya mvua ni mawingu!
 
kama yeye ndo anaamua kuwa muachane kwa nini usimwambie tu kuwa unaheshimu maamuzi yake na umwambie imetosha uone kama atathubutu kuendeleza wimbo wake wa tuachane, hata huo wivu hutausikia tena maana anakuchezea akili kwa vile anajua fika kuwa unampenda.
 
Anza mbele. Huyo hakupendi na anakutafutia sababu wewe huelewi. Lazimisha kuingia naye ndani ya ndoa utajaona cha moto.
 
ni "mchaga" wa wapi?...
 
Huyo dada ananipenda kufa wivu umemzidi mkuu mpaka inakera sana

Ulisahasikia wanaume wanasema jamaa anaibiwa mzimamzima sasa ndi hiyo unaibiwa mzimamzima unaona unapendwa... huyo mrembo wako anakuzuga hakuna kitu hapo piga moyo konde aanza maisha upya ingawa ni ngumu kuanza ila inabidi uyafanye hayo usijejijutia huko mbeleni....
 
sikiliza moyo wako unavyokuambia,ila sikushauri uendelee naye.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…