Yamoto band kumualika Rais Kikwete kuzindua nyumba zao

Nukta5

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2014
Posts
1,182
Reaction score
1,288
Mwanzilishi na mmiliki wa kundi la Muziki la Yamoto band pamoja na TMK Wanaume Said Fella amesema atamualika na kumuomba rais Kikwete kuzindua nyumba za kisasa za vijana wa Yamoto band ifikapo mwezi July. Hayo amesema kwenye birthday ya mmoja wa kundi la yamoto ambaye ni kiongozi wao kundi hilo ambae anafahamika kama Asley. Hongera sana Fella kwani pia hata Nature, Chege na Temba ulihakikisha wanamiliki nyumba zao zaidi ya moja kila moja.

source: Said Fella kumuomba Rais Kikwete kuzindua nyumba za kisasa alizowajengea Yamoto Band – Bongo5.com
 
Yuko sahihi kabisa Fella kumualika msanii 'mwenzao' JK wa ajili ya ufunguzi wa nyumba hizo za hao vijana wasanii wa Yamoto Band.

Fela atakuwa amefanya the right choice, kwa kuwa tulimsikia mkulu wakati anahutubia kilele cha Mei mosi kule Mwanza, akibainisha kuwa by nature, yeye ni msanii, na kama asingeukwaa Upresidaa, angekuwa msanii wa Bongo fleva, na anaamini angekuwa anafanya kolabo za nguvu na wasanii Diamond na Ali Kiba!
 
Huku ni kumshusha hadhi rais wetu jamani! Kama akienda kuzindua basi tusishae akialikwa kwenda kuzindua mhhhh bora nibaki nalo moyoni tu.
 
Hivi nyumba za kuishi znafanyiwaga uzinduzi kweli.?
 
mimi hayo ya kuzindua watajijua wenyewe, cha maana nilichoona ni hilo swala la nyumba kama ni kweli kawajengea nyumba ntampa respect Fella, maana wale watoto walivyopiga hela mwakajana na mwakahuu wakifulia lawama zote tutampa yeye
 
Ziwe Nyumba kweli basi sio ilimradi Nyumba kama alizokuwa anawanunulia Temba na Chege

Raisi naye kawa mtu mwepesi sana, Ikulu imekuwa sehemu nyepesi mnoo
 

Hii habari kama sijaielewa vile ina maana mwajiriwa Fella anawajengea nyumba maboss wake!!!?
Basi atakuwa kawapiga sana so akaamua kuwapooza kimtindo
 
Duh twendeni na mwendo huu mpaka oktoba naona mpaka wale wenzangu washagundua pale sio patakatifu tena na wakaao pia wamekua rahisi kwa mwendo huu hawezi kupewa muda wa kujiuliza kwa nini shilingi inapoteza thamani.
Mleta mada naomba nikusahihishe kidogo Fella hajawahi kumjengea nyumba Nature isipokua Chege na Temba ni sawa,naweza kusahihishwa pia.
 
Mkuu nimekupata ila Fella huwa akihojiwa anasema alimchukua nature akiwa hana kitu na kumuacha akiwa na nyumba mbili
 
Bado RAIS tutasikia na baikoko wanamhitaji akazindue ngoma yao mpya na ngwasuma pia watamhitaji ktk uzinduzi wao mpya wa album yao.
 
yani kweli rais mzima akaimbe "una ramboo" halafu first lady anaitika "una muwaa" kweli? :becky:
 
Hizo Nyumba Zinafikia milioni 200 kila moja au ndio zile za milioni 15?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…