Yanayochangia ndoa kuvunjika

kibebii

Member
Joined
Nov 5, 2009
Posts
84
Reaction score
15
Wanandoa wengi sana wapo hatarini kuachana au kutengana na wengine tayari wameshapigiana stop ya usinijue, kila mtu kivyake

ni vyema tukajikumbusha mambo ambayo yanachangia sana kuvunjika na sintofahamu katika ndoa ili yasaidie kutuweka katika mstari.

1. kukosa mawasiliano
2. Tafsiri potofu ya jambo bila ya kumuuliza mwenza wako
3. Kusema uongo
4. kutoka nje ya ndoa
5. Kuruhusu ndugu kuingilia mambo yenu
6. Ugumu wa maisha
7. Tamaa ya maisha mazuri

Nawe unaweza ongezea,
 
ndo mana ndoa za wazee wetu zilidumu
 

"Nitakupenda kwa raha na shida"
 
kusomasoma msg za mwenzi wako nayo ni sababu kuu
 
Kuiga iga mambo. Mtu anayeiga iga hubadirika kutokana na "popular culture" na hivyo ni vigumu kudumu kwenye ndoa
 
Aina ya marafiki wasiofaa na kutaka kuiga style zao za maisha,huleta kero na kutoelewana!
na hii nayo ni hatari sana watu wanapenda sana nao waonekane matawi ya juu, matokeo yake wanakosa mwana na maji ya moto
 
  1. kushindwa kujielewa na kuelewa umuhimu wa mwenza wako
  2. kuwa na makundi yasiyo sahihi
 

8. Ufujaji.... yaani mke au mume kuwa mbabe kwa mwenzi wake
9. Choyo
10. Ghubu.....ulalamishi usio na sababu, yaani hata jambo dogo tu, litasemwa kutwa nzima au usiku kucha
11. Umbeya..... Kama ni mke kila siku kuwekewa vikao vya kusutwa...... hiyo haifai, na kama ni mume, anakuwa mtu wa majungu tu, na hana mawasiliano mazuri na jamii iliyomzunguka
12. Kujipenda kupita kiasi...........
13. Usengenyaji na kutoa siri za ndani kwa majirani........yaani hata mumeo au mkeo unamsengenya kwa watu.........aibu hiyo
14. kupenda ndugu wa upande wenu zaidi..........
15. kutumia muda mwingi kwenye starehe na kuisahau familia

naona hizi zinatosha kwa leo.....................
 
  • Kukosea katika uchumba, kwani si kila mwanaume/mke anaweza kuwa mme/mke wako.
 
Sms zina tatizo gani kama wote ni waaminifu. Tumrudie Mungu.
Unajua tatizo la sms kwa upande mwingine ni kubwa hasa kama hamuaminiani msomaji ana kazi ya kujirusha roho muda wote , huenda sasa hivi yupo na fulani au anafnya jambo fulani ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…