Yanayoendelea Kenya ni uthibitisho tosha kwamba Demokrasia kamili haiwezekani kwa nchi za Afrika

Katika Kaunti 47 ni kaunti ngapi zilifanya maandamano ya kusimamisha nchi?
Maandamano yameshika kasi katika maeneo yale yanayoungwa na mzee wa kitendawili na si Kenya as wide.Lakini huyo Raila mimi nashindwa kumwelewa kwa namna nchi ya Kenya inavyoendesha mambo ni tofauti kabisa na nchi kama Tz ambapo baada ya uchaguzi wa Rais kama hujaridhika na matokeo unapeleka mahakama ya upeo wanaona kama mshindi ni halali au la na alifanya hivyo na akabwagwa.Labda hoja yake ambayo ni halali ni hiyo ya inflation ya vyakula

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Democracy is a myth, hakuna nchi duniani inayoendeshwa kidemocrasia. Huo ni ushetani.
 
Nimekupa mfano hai wewe unasema tena 'kama', hiyo kama haijatokea, so ni possible kuwa na peaceful elections
 
Hana hoja, kipindi cha Uhuru vyakula ndio vilikuwa ghali zaidi kuliko sasa na akawaambia kundi la Ruto waache kumlaumu Uhuru
 
Mtu mweusi ana mafatizo ya kufikiri hasa Africa.

Fikiria Kenyatta na Raila ni maswahiba lakini Raila huyo huyo alikuwa anadai Kenyatta alimuibia kura mwaka 2017 na 2012. Sasa Kenyatta ilitakiwa atoke hadharani na kusema kama miaka hiyo alimuibia kura kweli Raila au la ili tupime maneno ya Raila. Lakini Kenyatta hazungumzii chaguzi hizo za nyuma bali anamchochea Raila kuwa mwaka 2022 ameibiwa kura na Ruto.


Hata hapa Tanzania hzo wapinzani wanadai matokeo ya uchaguzi yahojiwe mahakamani, lakini nakuhakikishia hilo likikubalika na kuingizwa katika katiba na ikitokea mahakama ikaamua kuwa mgombea wa CCM au mgombea mwingine ameshinda kihalali bado walioshindwa hawatakubali na wataingia barabarani.
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu kuhusu hawa wapinzani. Definition ya demokrasia kwao ni pale wanapopewa kipaumbele wao na maslahi yao kutoingiliwa hata kama wako kinyume na utaratibu.
Hivi kwa sasa lile dai la katiba mpya na tume huru ya uchaguzi imepotelea wapi baada ya kwenda ikulu kunywa sharubati? Hayatola alikuwa muumini wa dikteta mwepesi ili nchi iende lakini walivyoanza kuguswa maslahi yake tu,akageuza gia angani kudai katiba mpya.
Afrika hatuna viongozi wazalendo bali tuna vibaraka wa westerners.
 
Sasa kama hayo ya Kenya ndiyo maana ya Demokrasia badi hakuna haja ya kuyaona Tanzania Wala Rwanda .

Kenya itaanguka vibaya sana Kwa sababu ya kichaa mmoja anayeitwa Raila amabaye alitakiwa awe amepigwa risasi siku nyingi .

Kuwaacha watu hata mil. Moja hai na kuvuruga amani ya watu Mili. 50 ni ujinga mtupu.

Hatuungi mkono Wizi,ufisadi , ushoga, matizi mabaya ya serikali n.k. Raila alitakiwa atuambie kuwa Ruto amefanya ufisadi wali na amaina fedha kiasi Gani za umma n.k. hapo tungemuunga mkono lakini Kwa Sasa Hana sababu yoyote zaidi ya kutaka kuonyesha kuwa ana watu na anaweza kuvunja amani ya nchi. Hivi wajaluo wakivunja amani wanategemea nchi ya Kenya itakua salama. ?
 
Demokrasia haiendelei Afrika kwa sababu ya ubinafsi....mfano Kenya na Afrika ya Kusini viongozi waliochaguliwa ki demokrasia hawajaleta mabadiliko hitajika zaidi ya kufanya 'nepotism' fikiria kiongozi mkubwa serikalini anadiriki kusema serikali ni kama kampuni hivyo wenye hisa lazima washibe kwanza
 
Na hii ni dalili njema, wenzetu wanajaribu wakati sisi tunaogopa hata kujitetea na kusubiri huruma ya watawala.....
 
Narudia Tena, demokrasia kamili haiwezezekani Africa
hakuna kitu kinachoitwa demokrasia hapa duniani, wala hakuna kitu kinachoitwa demokrasia kamili popote duniani,......

kinachotokea ni wakoloni kulazimisha mifumo yao ya utawala iliyofeli kwao sisi tuifuate, ni ujinga na upumbavu kujaribu kuiga aina hii ya mfumo wa utawala!

afrika, kama ilivyo Asia ina mifumo yake inayofaa, sio huu unaoitwa demokrasia na makandokando yake!

angalia, hata ulaya na amerika ya kaskazini nako huu mfumo umeshafeli,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…