Yanayoendelea ligi ya Misri ni funzo kwa watanzania hasa Simba S.C na mashabiki wao

Mhimili uliojichimbia

Senior Member
Joined
Jul 2, 2017
Posts
172
Reaction score
191
Ukiangalia hiyo table utagundua vitu kadhaa
1. Timu zinazoshiriki club bingwa na zimeingia 16 bora zote hazifanyi vizuri kwenye ligi ya ndani ya Misri( Al-ahly no7 na Ismaily ya mwisho no 16). Hii inaonesha inahitaji nguvu ya ziada kushiriki kwa ubora kwenye vikombe vingi kwa wakati mmoja.

2. Suala la vipolo sio ligi ya bongo tu naona wa Misri nao vipolo kibao wakati A-ahly akicheza mechi 11 na Ismaily mechi 13 kuna timu zimecheza mechi 19.

3.Hao wa Misri watatumia nguvu kubwa sana kupigania ubingwa wa CAF champions legue kwa kuwa ligi ya ndani ni tia maji tia maji, hivyo maandalizi ya Simba yanahitaji nguvu ya ziada.

USHAURI KWA SIMBA:
Kwenye michuano ya mapinduzi wapeleke kikosi kilichocheza na mashujaa au wajitoe kwa manufaa makubwa ya baadaye.
 

Attachments

  • Screenshot_20181227-111908_CM%20Browser.jpeg
    59.2 KB · Views: 25
Ndivyo, Inavyotakiwa, hao vijana wa mashujaa wacheze hizo ndondo.
Tunataka kuingia robo fainali za mabingwa kwa sasa.
Kama ubingwa wa bara hata Mtibwa walishawahi kuchukua miaka ile.
Maoni mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…