Yanayoendelea mtaani kwetu

Yanayoendelea mtaani kwetu

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Huu mtaa naupenda sana maana huwa haukosi amsha amsha.

Jirani yangu hapa ni mstaafu basi ukiamka tu kwenda kupambana huko utakuta kakaa nje ya uzio wa nyumba yake, basi lazima akusimamishe muongee ataishia kukubomu tip kwa ajili ya kwenda kwa mangi ili "aamke".

Ukishamalizana tu na mstaafu, utawakuta vijana wa kitaa kwa mangi nao wanashtua, lazima utasimama utawapa salam ikiwezekana utawatoa au utawalilia njaa halafu utawaaga uende zako.

Ukimalizana na vijana dukani kwa mangi, utapita karibu na uwanja sasa utakuta vijana wanapasha hapo wakijiandaa kwa mechi, nao wanaweza kuja kukuambia broo tuachie ya kununulia maji baada ya mazoezi, unaweza kuwaachia au ukawalilia njaa, ila kama ukiwaachia basi wanaweza wasinunue maji bali wakanunulia cha Arusha.

Nampenda mno mwenyekiti wangu wa serikali za mtaa, kwakua anatufahamu wakazi wake wote, kwa majina , kazi zetu pamoja na namba zetu za simu, ukikutana nae lazima atakupa wosia mreefu kuhusiana na maisha kwa ujumla akisisitiza mno kushiriki kwenye masuala ya ujenzi wa taifa.

Ikifika ijumaa jioni basi ni shangwe pale dukani kwa mangi. Kwa kifupi mangi huwa anafanya biashara, na ule uwanja unageuka parking za wadau toka maeneo mbali mbali.

Kwa uchache tu, hayo ndio yanayojiri mtaani kwangu, karibu unieleze yanayojiri mtaani kwako pia.
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Ngoja mangi apige hela.....
Ukiona watu hawatumii akili zao vizuri, basi zitumie wewe.
 
Back
Top Bottom