Yanayoendelea ya Fei Toto huko TFF

Yanayoendelea ya Fei Toto huko TFF

Mributz

Senior Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
177
Reaction score
527
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jana Mei 4, 2023 ilisikiliza shauri la mchezaji Feisal Salum 'Feitoto' aliyewasilisha malalamiko akitaka kuvunja mkataba na waajiri wake Young Africans kupitia barua yake ya tarehe Machi 6, 2023.

Baada ya kupitia na kutafakari kwa kina hoja zote za pande husika, Kamati imetupilia mbali maombi hayo kwa msingi kwamba ilishaamua juu ya uhalali wa Mkataba wa Mchezaji huyo na klabu yake kwamba ana Mkataba unaoendelea mpaka 2024.

Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazotawala uvunjaji wa mikataba ya wachezaji inayoendelea, mchezaji ni lazima aanze majadiliano na Klabu yake ambayo ndio yenye haki nae.

Uamuzi kamili kwa pande zote mbili zilizokuwa zinahusika katika shauri hilo utatolewa baadae kwa pande husika kujulishwa.
 
Hivi kwanini fei asiende kuonana na uongozi wa Yanga ili wamalize hii ishu?
Mbona ni kama jamaa anapoteza career yake aloijenga for so long long kirahisi hivyo?
Au alienda wakagoma kuongea nae?shida iko wapi?nani mshauri wa huyu kijana?
 
Hivi kwanini fei asiende kuonana na uongozi wa Yanga ili wamalize hii ishu?
Mbona ni kama jamaa anapoteza career yake aloijenga for so long long kirahisi hivyo?
Au alienda wakagoma kuongea nae?shida iko wapi?nani mshauri wa huyu kijana?
sikio la kufa. mchezaji kalewa sifa
pia mawakili wachumia tumbo wanaolazimisha kushauri ili waendelee kupiga hela
 
Back
Top Bottom