Mpaka leo Mwili Rais Mstaafu Edgar Lungu haujazikwa kisa ni mgogoro kati ya familia ya Rais Mstaafu Lungu na serikali ya Rais Haikainde Hichelema.
Familia inasema marehemu Rais mstaafu aliacha wosia kuwa siku akifa Rais wa sasa asisogelee jeneza lake.Siku za maombolezo zimeisha bado utata upo kiasi kwamba imemlazimu mwanasheria mkuu wa serikali ya Zambia kwenda mahakamani South Afrika kupinga mwili wa Rais mstaafu Lungu usizikwe South Afrika leo kama familia ilivyopanga.
Kwa upande wake Rais wa sasa wa Zambia Hichelema anadai pamoja na kuwa Rais Lungu alimtesa na kumweka kwenye death row jela huku akiwa na kesi ya uhaini (kama Tundu Lissu) lakini yeye hakumuondolea Kinga Rais huyo mstaafu kama watangulizi wake walivyofanya.
Anyway to make a long story short ni kuwa chanzo cha yote hayo ni uhasama na vitimbi vya kisiasa baina ya Rais Mstaafu Lungu na Rais wa Sasa Hichelema.
Haijawahi kutokea Rais wa nchi kuzikwa nchi nyingine kisa tu ni uhasama wa kisiasa. Isitoshe Zambia ni nchi yenye wakristo wengi na Marais wote ni Wakristo. Yanayotokea ni matokeo ya kanisa kushindwa kusimamia haki tangu awali.
Kama Taifa tujifunze maana na sisi huu utekaji, kesi, mauaji yanayotafrisiwa kuwa na mrengo wa kisiasa yanajenga uhasama mkubwa siku zijazo. Ni Trauma tunatengeneza.