UPDATES: 1
Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima, Serikali imefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini kuwa tukio hili lilitokea Januari 10, 2023 kwenye Shule moja ya Msingi iliyopo Wilayani Kyerwa, Kagera.
Akithibitisha hayo kupitia Akaunti yake rasmi ya Mtandao wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kuwa hali ipo kwenye udhibiti mzuri (Situation is under control) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atatoa taarifa inayohusu tukio hilo Januari 25, 2023.
Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na amewaasa walimu kuzingatia utaratibu wa adhabu wanazotoa kwa wanafunzi, pia amewataka kuheshimu sheria kwani Hatua kali zitachukuliwa kwa wale watakaofanya aina hii ya ukatili.
Your browser is not able to display this video.
UPDATES: 2
Mwalimu aliyeonekana akimuadhibu mwanafunzi kinyume na taratibu, akimchapa kwenye nyayo za miguu, amesimamishwa na kutenguliwa Kwa nafasi yake kama Mwalimu mkuu. Pia, ameshaandikiwa Mashtaka kwa Mamlaka ya TSC ili akajibu tuhuma zinazomkabili.
Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
UPDATES: 3
Mtuhumiwa yupo ndani, Mkuu wa Mkoa ameshafika hospitalini kumuona mtoto na Jeshi la Polisi linaendelea na hatua zake.
Sasa mtoto kama huyo atakuwa amefanya kosa gani mpaka anapewa adhabu kama hiyo kisa kapata 1/10 au
Na pembeni kule wamekaa wengine wanacheka tu kama ni jambo la kawaida linalotendeka 🚮 kuna watu ni matakataka
Mm siwez nikawa hapo staff nikavumilia icho kinacho tendeka....ova!
Japo sometimes hao watoto wanaweza kukupiga tukio mpka ukapanic.....
Mbona wazungu walisha abolished Stick in their school....
All in all Mungu ni mwema na Mwaminifu wakati wote.....
so sad
unakuta mwalimu katoka kuachana na mumewe alafu ahsubui anaingia ofisini
whata do you expecting
ila hata kama unastress vipi huwezi kumfanyia hivo mtoto wa mwenzio !!!
watu kama hawa inatakiwa ndo wawe wa kuwafanyia mfano ili kenge wengine wenye tabia kama hizi wasijitokeze
Sasa mtoto kama huyo atakuwa amefanya kosa gani mpaka anapewa adhabu kama hiyo kisa kapata 1/10 au
Na pembeni kule wamekaa wengine wanacheka tu kama ni jambo la kawaida linalotendeka 🚮 kuna watu ni matakataka
so sad
unakuta mwalimu katoka kuachana na mumewe alafu ahsubui anaingia ofisini
whata do you expecting
ila hata kama unastress vipi huwezi kumfanyia hivo mtoto wa mwenzio !!!
watu kama hawa inatakiwa ndo wawe wa kuwafanyia mfano ili kenge wengine wenye tabia kama hizi wasijitokeze
Ebu mfutilieni mwalimu YUSUPHU PANGOMA na mwenzie mmoja kama ana mguu mbovu anatembea na gongo la chuma ni walimu wa kuigwa wanaishi poa sio hao washamba wakishavaa hayo maviatu makubwa wanakanyanga mwanafunzi kama anataka kuchinja mbuzi.
Mwalimu PANGOMA na mwenzio yule mweny mguu mbovu watu safi kabisa wanajielewa huko Mara wanafunzi wanawapenda sana na wamekuwa msaada mkubwa sana kweny jamii zao..Sio huyo anataka kuogopewa ni ushamba.
Daah aisee yàaani kiukweli ndugu zetu walimu nyie nadhani miongoni mwenu kuna baadhi yenu ni vichaa ka.a si kurogwa kabisa asee
Maana kwa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kufanya ukatili na ujinga kama huu yaani mwanaume mwenye akili timamu unawezaje kumfanyia mtoto unyama na ukatili wa kiwango hiki tena mtoto mdogo kabisa ambaye daah ata sijui kakosa nini lakini mmmh
Nadhani serikali inapaswa kufanyanya juhudi nyingi sana hasa za kisaikolojia ya hawa wenzetu walimu ili wawe timamu kichwani asee.
Kiukweli inasikitisha sana mpaka nimeshindwa ata kuiweka apa iyo video alafu cha ajabu kabisa yaani walimu wenzake na uyo mwalimu anayefanya unyama wako wanamwangalia tu mwenzao na kufurahia unyama anaoufanya daah ama kweli.View attachment 2494438View attachment 2494439