Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
PICHA NA MATUKIO YA UZINDUZI WA ILANI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI
Mgeni rasmi ni Kiongozi wa Chama Semu Dorothy
====
Semu Dorothy; "Leo tunazindua ilani. Kwa hivyo ni siku ya kihistoria katika nchi yetu; siku ambayo inaweka utamaduni mpya wa kisiasa katika kuendea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Uchaguzi huu hatuendi kuukabili kwa maneno matupu."
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Ndugu Semu Dorothy akizindua Ilani ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Ilani hiyo imezinduliwa leo Novemba 17, 2024 katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema Makao Makuu ya ACT Wazalendo Magomeni Dar es salaam.
"CHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza kusikitishwa na mwenendo wa usikilizwaji wa rufani za wagombea ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.
Mchengerwa aliagiza utekelezaji wa agizo kufanyika kwa mapitio ya kuenguliwa kwa wagombea.
Kupitia taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Isihaka Mchinjita, amesema tathmini waliyofanya imebaini kamati za rufani zimeendelea kuwaengua wagombea wao.
Amesema hata pale ambapo makosa yaliyojitokeza yalikuwa madogo, hayapaswi kuathiri mchakato wa uchaguzi.
Mchinjita amesema wagombea wao kutoka majimbo mbalimbali, yakiwamo Tandahimba (500) Newala Vijijini (93), Kinondoni (80) na Bukoba Vijijini (621) wameenguliwa licha ya maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mchengerwa, yanayotaka kuzingatia haki na kuepuka kuadhibu makosa madogo yaliyojitokeza.
Mchinjita amesema chama hicho kinalaani ucheleweshaji na kutochukuliwa hatua stahiki kwa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo mengi kwa kushindwa kufanyia kazi maelekezo ya kuwasilisha fomu za uteuzi ili kufanya marekebisho kwa wagombea walioenguliwa.
Kutokana na hali hiyo, amesema wanamwomba waziri mwenye dhamana kusimamia utekelezaji wa agizo lake kwa kuhakikisha haki inatendeka.
“Tutamwandikia waziri orodha ya maeneo ambayo agizo lake halijatekelezwa kikamilifu pamoja na vielelezo husika.
“Tutachukua hatua za kisheria zikiwamo kufungua kesi mahakamani kupinga uamuzi wa kuwaengua wagombea wetu ili kuhakikisha uchaguzi unarudiwa katika maeneo husika,” amesema.
BONYEZA HAPA KUSOMA ILANI YA ACT WAZALENDO 2024 SERIKALI ZA MITAA