Yanayojiri: Uchaguzi wa Marudio Kenya - Oktoba 26, 2017

Amani tafsiri yake ni ipi kama kila anayesema ukweli anapigwa risasi na kuuliwa?, huo ni utulivu lakini Kenya hakuna amani

Huwa nashangaa MACCM mnavyo onekana kujali sana kuhusu demokrasia ya Kenya na kujifanya watetezi ilhali huko kwenu madudu, mumekandamiza upinzani. Huku tunamuuguza jamaa wenu mliyempiga risasi 38 kisa anahoji, mara taarifa za miili 15 kwenu inapatika kwenye viroba inaelea kwenye fukwe, Maiti 15 Zaopolewa Zikiwa Kwenye Viroba - Global Publishers
Yaani matukio mengi ya kiajabu na mauaji ya kimya kimya lakini unatumia nguvu nyingi kukesha huku ukihangaika kuongea kuhusu matukio ya Kenya na kujifanya mwanademokrasia. Kwenu hata kiongozi wa upinzani kuhutubia watu watano tu kosa la jinai, Raila angekua hapo kwenu mngekua mshamnyofoa mapum.bu
 
Mzee tunawaombea mpite salama katika kipindi kigumu. Hakuna anayependa machafuko labda shetani. Mkishamaliza uchaguzi salama tunaomba muanze kuumaliza ukabila. Hiyo sumu inaendekezwa sana na haina mashiko katika karne hii. Walau mjitahidi kuoleana, ingawa najua mwanamke wa Gikuyu bado anaogopa Mkono wa Sweta!
 
Ni kweli kabisa suala la Lisu serikali haiwezi kukwepa lawama, ila maiti zinazookotwa baharini, hadi leo hakuna familia wala mtu yeyote aliyejitokeza kupotelewa na ndugu yake, dalili zinaonyesha kwamba maiti ni za wakimbizi wa ethiopia wambao huwa wanafungiwa kwenye containers wakisafirishwa kwenda South Africa, siku za nyuma maiti nyingi zilikuwa zinaokotwa porini, lakini siku hizi hakuna tena maiti zinazookotwa porini ila bado wanakamatwa kwa wingi mipakani.

Ila hata kama ni watanzania lakini ni wazi kuwa sio mauaji ya kisiasa kwa sababu ukiondoa Ben Sanane hakuna chama chochote cha siasa kilicholalamika kupotelewa na viongozi au wanachama wake, ukiondoa Lisu, niambia nani mwengine aliyeshambuliwa au kuuliwa?, ila Kenya kuanzia August 8 hadi leo wanaojulikana ni zaidi ya 70, hadi viongozi wa dini wanauliwa kinyama, hopeless country.
 
Vile vituo vilivyokosa watu asubuhi vipi wameshaanza kupiga kura??
 
Huko hamuwezi huu mtiti, hebu niambie kama Lowassa au Mbowe athubutu kufanya anayoyafanya Odinga, atanyofolewa maken.de na viungo kama albino. Huko muendelee kuishi hivyo labda mtaokolewa siku ya kiama.
Bado unakataa ukweli kwamba Kenya mnauwa watu wengi bila sababu za msingi, na hili jambo la kuua watu halijaanza leo, ni tangu enzi za mzee Jommo Kenyatta na linaendelea hadi leo, la ajabu linaanza kuzoeleka katika jamii ya Kenya, juzi father kule Kisumu ameuliwa, no one talks about him, ingekuwa Tanzania makelele yake yasingewezekana kwa sababu hayo ni mambo mageni huku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…