Yanayonikuta London, Uingereza - Part 2

Kwamba hata kama 'network' yake inayumba Tanzania ndiyo kuna doctors na medical facilities bora kuliko England? Kurudi TZ si suluhisho tena itakuwa ndiyo anazidi kujididimiza, bora apambanie afya yake(mental or physical or both) akiwa hukohuko.
Wanakwambia karogwa saaa UK atapata mganga wa kupiga manyanga amuague
 
Hakunaga mgonjwa wa akili anayekubali kuwa ana tatizo
Lakini maelezo yako tu yanaonyesha hauko sawa,tafuta tiba jomba
Nilijua nikikwambia unionyeshe ni wapi pamekufanya unione nina ugonjwa wa akili nitakuwa nina kuonea. Uwezo wako ndio umeishia hapo.

Nimeshaandika hapo juu. Mimi nilishanya kazi kwenye mental health settings. Ninajua umuhimu wa ku seek for help kama una tatizo la afya ya akili. Nimeshaona hadhari za watu waliokataha kwa muda mrefu. Halafu mimi sioni unyapaa wowote.
Miaka ya nyuma sana, mimi kuna kipindi nilikuwa nina struggle na mental health na bado nikiwa kazini na wala hakuna aliyejua chochote. Nikamwambia doctor wangu bila kushauriwa na mtu yoyote na alisaidia.
Halafu miaka yakaribuni. Nilishaomba niwe access kama nina any disabilities. Lakini nikatolewa nje kiaina. Kwa hiyo kwangu sio issue.
Hata huyu doctor kama angeniambia kwamba una tatizo bila kuweka uongo kwenye report. Nisingelalamika.
Tatizo ni yeye kuandika uongo kwenye report.
 
Mimi na wewe wote tuna tatizo la akili
Kuna miaka ya nyuma hapa JF watu walikuwa wanashusha nondo sana. Kama mtu akikuita chizi anatoa sababu kwa nini amesema hivyo. Those days are long gone.
Sasa kuna viazi mviringo kibao
 
Rudi kwenu katibiwe
 
Ubishi wangu ni upi. Doctor kwenye report yake kanilisha maneno. Halafu mimi nikubali kwa sababu ya kuonekana mbishi.
Wewe utakuja kuliwa kwa kuogopa kuoneka mbishi.
You will be fine. Ukija nenda moja kwa moja Mirembe ukatibiwe.
 
Kwa vyovyote vile wewe utakuwa na ugonjwa mkubwa wa akili (schizophrenia), maelezo yako yanaakisi hilo. Kwa mfano;
1. Kuhisi watu wengi wanaokuzunguka ni maadui zako na wameungana dhidi yake.
2. Kuhisi kuna namna mazingira yako yanajihusisha kukudhuru.
3. Kuhisi watu fulani fulani wanakufuatilia kwa nia ovu dhidi yako.
4. Kujisikia vitu visivyo vya kawaida vinakuchoma choma na wewe kuvitengenezea nadharia isiyoweza kuaminiwa.

Ni vyema ukamuona Daktari wa magonjwa ya akili tu.
 
Wewe ni baadhi ya viazi mliojazwa hapa. Mpeo wenu wa akili unaishia kurudia mambo kama kasuku.
Malizia hadithi basi
Mbona unakuwa mkali
Jibu hoja zako tu
Umeleta hadithi lazima ukutane na maswali na pia majibu
Usikasirike kwani unatafuta sympathy humu au

Ulitaka upewe pole nyingi au
Dr Shika story yake ilikuwa kweli
 
Malizia hadithi basi
Mbona unakuwa mkali
Jibu hoja zako tu
Umeleta hadithi lazima ukutane na maswali na pia majibu
Usikasirike kwani unatafuta sympathy humu au

Ulitaka upewe pole nyingi au
Dr Shika story yake ilikuwa kweli
Wewe kubali. Hauna uwezo wa kujenga hoja
 
Kwa vyovyote vile wewe utakuwa na ugonjwa mkubwa wa akili (schizophrenia), maelezo yako yanaakisi hilo. Kwa mfano;
1. Kuhisi watu wengi wanaokuzunguka ni maadui zako na wameungana dhidi yake.
Afadhali hata wewe umejenga hoja. Nina heshimu mchango wako.Lakini mbona umeruka kilichonifanya kufungua hii thread.
- Pia hii ya kuhisi watu wengi wanao nizunguka ni maadui. Mbona sijamtuumu doctor (GP). Kuna watu hapa wamesema umelogwa na ndugu zako. Nikawambia hayo ni uongo. Mbona sijalalamika kuhusu Watanzania nilikuwa ninaishi nao London. Huyo doctor niliyemtuhumu nimeweka sababu.
2. Kuhisi kuna namna mazingira yako yanajihusisha kukudhuru.
Sijui una refer kipi. Lakini nina amini mawasiliano yangu yanakuwa monitor bila idhini yangu. Kwa hili nina achia muda kuwa judge.
3. Kuhisi watu fulani fulani wanakufuatilia kwa nia ovu dhidi yako.
Kufuatiliwa ndio mfano huu. Hapo ni kwenye picha nilikuwa nimekaa Mcdonalds. Gari ya Polisi ikaja ikawa ime pack nje. Yaani pale nilipokuwa nimekaa na wao walkpokuwa wamepaki gari mara ya kwanza, kuna ubao ulikuwa una block view ya wao kiniona. Wakazogeza gari upande wa kushoto kwangu ambapo wangeweza kuniona. Wakabaki kwenye gari muda wote niliokuwa nimekaa Mcdonalds.
Nilipondoka nao wakaondoka. Nilikuwa na clips kibao za matukio kama haya.

Picha namba 1: Hapa nilikuwa nimekaa McDonalds. Mara ya kwanza walikuwa wame pack gari kulia kwangu. Lakini hiyo white board ya Mcdonals ikawa ina block view. Baadae waka move gari upande wa kushoto. Na mimi hapa nilikaa Mcdonals kwa muda mrefu na pia wao walibaki kwenye gari kwa muda mrefu.

Picha namba 2: Hapa nilikuwa nimetoka nje ya Mcdonalds kuelekea nyumbani na wao wakaanza kuondoka.


Picha namba 3: Na wao pia waliondoka. Hapa nilikuwa nina tembea kwenye pavement na wao pia wapo nyuma yangu. Utaona kabisa hapo wame position gari ku face nilipokuwa nina tembea labda walikuwa wanachukua picha.
Sina criminal record yoyote kwa miaka yote niliyoishi hapa UK. Na pia Polisi hawajawahi kuniambia kama kuna tatizo. Ningeweza kukuwekea matukio kama haya kibao

4. Kujisikia vitu visivyo vya kawaida vinakuchoma choma na wewe kuvitengenezea nadharia isiyoweza kuaminiwa.
Hii ambayo nina jisikia kama electrical shock kwenye mwili ilianza mwaka jana. Na muda unavyokwenda nina sikia kwa nguvu zaidi. Hii kama sharp needle pain hai tokei mara nyingi kama hiyo electrical shock. Hii siwezi kutoa ushahidi wowote zaidi ya kusema ninavyojisikia. It is what it is! Na ndio imechangia kwa asilimia kubwa ya decision yangu ya kurudi Tanzania kwa sababu they are affecting my well-being.
Ni vyema ukamuona Daktari wa magonjwa ya akili tu.
Niambie nimwone dokta kwa lipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…