Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Polisi kuua raia hovyo
- Mawaziri na viongozi kufanya na kusema watakacho
- Jumuiya za kidini kugomea sensa bila kujali
- Ufisadi wa kutisha nchini unaoendeshwa bila woga
- Migongano ndani ya CCM kufikia hatua ya kutishiana kwa bastola
- Usalama wa taifa kuhusishwa na utekaji wa watu
- Wawekezaji wa nje kuonekana wana mamlaka zaidi ya raia
- Bunge na Spika kukosa heshima inayostahili
- Kamati za bunge kupokea rushwa
- Nchi jirani kututikisia kiberiti juu ya suala la mipaka
- Ofisi zetu za ubalozi kutothaminiwa
- Kuwa na migomo ya wafanyakazi kila kukicha
- nk, nk
Yote haya ni matokeo ya kuwa na ofisi ya uraisi isiyoheshimika na watu wenye madaraka kuona kama kuna "vacuum" ya uongozi, na kujua kwamba hata wafanyeje, sio rahisi kwamba watachukuliwa hatua (can get away with it). Ni kama vile nchi haina raisi mwenye mamlaka, kwa sababu wengi wanaona kilichopo ni ubabaishaji (uswahili) tu.
Amini nawaambieni, tushukuru Mungu hatuko enzi zile za majeshi barani Afrika kupindua nchi.