YANGA AFRIKA, NINA MASWALI TATA, LABDA KWA SABABU UELEWA WANGU MDOGO.

YANGA AFRIKA, NINA MASWALI TATA, LABDA KWA SABABU UELEWA WANGU MDOGO.

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
.
Swali langu la kwanza ni, lengo mama kabisa msimu huu lilikuwa ni lipi?? Najua jibu litakuwa, 'Kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kupata nafasi ya kushiriki klabu bingwa mashindano yajayo'

Swali la pili litakuwa, 'Mikakati gani iliwekwa kuhakikisha lengo mama linafikiwa?' Naweza nisiwe na jibu sahihi lakini naweza kubuni, marekebisho muhimu yalifanywa kikosini, kuanzia kwa wachezaji hadi kwenye benchi la ufundi.

Hili jibu linaweza kuzua maswali mengine yatakayokuwa vipengele vya swali la pili. Mosi, Wachezaji waliokuja, je ni kweli wana uwezo wa kukupa ubingwa?? Pili, Je wanaendana na falsafa ya timu?? Tatu, una hakika watazoeana ndani ya muda ambao watakuwa tayari kukupa ubingwa??

Tuseme hayo yote majibu yake ni ndiyo. Swali langu lingine linakuja, Umewatazama wapinzani wako wa karibu na kujiaminisha kuwa unaweza kuwashinda kwenye vita ya ubingwa??

Tuseme nitajibiwa tena, NDIYO. Nitaguna halafu nitauliza, Mmeitazama Simba lakini?? Kumbuka pale juu nimesema 'kwa uelewa wangu mdogo'. Najua mnafahamu kuliko mimi.

Hapo nitaulizwa, Je naandika haya kwasababu Yanga amefungwa kwa mara ya kwanza?? Nitajibu Hapana! Kufungwa siyo dhambi. Je kufungwa na Coastal kunaweza kuwatoa Yanga kwenye mbio za ubingwa?? Nitajibu Ndiyo. Ndiyo kama watachagua kuyaishi haya matokeo, ndiyo kama watashindwa kupata majibu ya kwanini hawafanyi vizuri??

Swali langu la mwisho litakuwa, Je Yanga Afrika mnapaswa kuumia kama mtakosa ubingwa mwisho wa msimu?? Nitawasaidia kujibu, Hapana. Kwanini?? Kwasababu ya majibu ya maswali niliyouliza kabla.

Si rahisi kuchukua ubingwa katika mazingira waliyopo Yanga msimu huu, nasisitiza Sijasema HAIWEZEKANI, nimesema, SI RAHISI. Ugeni mwingi kikosini, aina ya wachezaji na Nature ya Simba ambaye ndiye mpinzani wa karibu, ndiyo sababu zangu.

Nadhani ni vema, Yanga ikatulia na kujipanga zaidi badala ya ku'panic' kwa kupoteza rekodi ya 'Unbeatean' au kama itakosa ubingwa mwisho wa msimu. Tukumbuke Tanzania tunaweza kuingiza timu nne mashindano ya Afrika msimu ujao. Kama hili litatokea, bado Yanga watakuwa hawajapoteza lengo mama.

Napokea maoni 'BILA MATUSI'[emoji120].
deo_mwanasoka-___CMDN168gX8K___-.jpg
 
Mkuu unakadi ya uanachama wa Young African sports club?
Je kadi ni hai?
Nauliza tu Mkuu!
 
WACHAMBUZI WA BONGO! Timu ikishinda itamiminiwa sifa zote, ikifungwa itasemwa maneno yote! Hii hii Yanga ikifanya vizuri hutasikia upu- uzi wanaongea sasa!
 
Yanga imeanzishwa tangia miaka ya uhuru, lakini cha kushangaza mwaka 2021 eti ndo wanachangishana pesa ya kuweka vitanda na magodoro klabuni,tena kwa kudunduliza kwenye bakuli la mchango.
 
Back
Top Bottom