Yanga bado ina safari ndefu ya kujifunza

Peramiho yetu

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2018
Posts
5,303
Reaction score
14,983
Kiukwel mashindano ya CAFCL na CAFCC ni mashindano yenye hadhi yake kwa vilabu.

Ndiyo maana Simba imeonja utamu wake na haipo tayari kuyapoteza kirahisi, wana mbinu za kukaribiana na fitina zozote.

Juzi Simba walienda Angola siku moja kabla ya mechi, si kwamba hawana pesa hapana. Intelejinsia yao iliona kuna harufu ya hujuma.

Sasa ndugu zangu Yanga wao waliwapokea washindani wao na kuwapa kila aina ya msaada, eti wakidhan huo ndiyo uungwana katika mpira. Hakuna kitu walibugi kama tendo hilo.

Mshindani wako lazma aone joto la mashindano, ahisi kweli yupo ugenini siyo nyumbani. Kwa kufanya hayo unakuwa umemchanganya kihisia na kuhisi joto la pambano.

Sasa leo tunasikia huko Al Hilal hataki mechi kuoneshwa wala kutangazwa kwa radio, sisi huku mashabiki roho iko juu, akili zimeturuka, hatujui itakuwaje! Ndio wale tuliowapokea kwa bashasha tele wanatufanyia haya?

Binafsi naona Yanga ni klabu ya kufurahisha mashabiki wao kwa kuwekeza kwa waandishi wa habari waiongelee vizuri na si kuonesha madhaifu ya timu yao.

Ukiangalia Simba toka mwanzo utaona umakini walionao wenzetu. Wameenda Misri sisi tulibaki mji wa Avic, walienda Sudan sisi tulibaki mji wa Avic, walienda Zanzibar sisi tulibaki mji wa Avic!

Wamecheza na Al Hilal, Asante Kotoko, Kipanga sisi tulicheza na Mbuni Transit Camp!

Ukiangalia huo mlolongo utaona kabisa klabu yetu bado ina safari ya kujifunza

Si vibaya kujifunza na tusitarajie makubwa kupitia mashindano haya.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…