Yanga bila kurekebisha haya mechi ya kesho itakuwa ngumu

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Kesho Yanga watatupa karata yao dhidi ya Club Africain ya Tunisia. Kwangu hii ni mechi ngumu kuliko ile ya Al hilal. Yafuatayo ni mafungufu ambayo km kocha hajayafanyia kazi basi itakuwa ngumu kusonga mbele.

1.Kutengeneza mashambulizi kwa taratibu( slow). Warabu wakiwa ugenini huwa wanapenda kuipoozesha "game". Sasa km Yanga wataingia na staili ya "slow" km tulivyowazoea basi biashara itakuwa imeisha.

Yanga wanatakiwa kushambulia kwa kasi Ili kuweze kupata ubora wa Morison anaependa mpira wa nipe nikupe kwa kasi hapo ndipo huwa anapata mwanya wa kulazimisha timu pinzani kufanya makosa na kuweza kupata penalt au faulo nje ya 18.

2.Wawe makini na shambulizi la kushitukiza( Counter attacks). Mechi mbili na Al hilal Yanga walifungwa magoli mawili yanayofanana tena na mchezaji mmoja. Goli la Okra dhidi ya Simba ilikuwa ni counter pia. Ni km kocha ameshindwa kuwaelekeza wachezaji jinsi ya kuchukua tahadhari wakati wanapoenda mbele kushambulia. Kwenye Counter shape ya timu huwa inakaa ovyo (Shaghalabagala).Wachezaji wanaenda kukaba huku wamerundikana km mafungu ya nyanya. Wakipigwa chenga wote wanapotea. Na nadhani Club Africain watakuwa wamezifatilia kwa makini mechi za Yanga na kubaini haya niliyoyasema.

3. Udhaifu sehemu ya kiungo mkabaji na beki wa kati. Hili kila mtu analijua hakuna haja ya kuongea sana.

4. Mashambulizi yote kupitia kwa Mayele. Unapomtegemea mchezaji mmoja ndo afunge unairahisishia timu pinzani kuunda mkakati wa kumzuia hasa unapokutana na timu bora.Simba kwa mfano asipofunga Mosses Phiri Chama,Sakho,Okra, watafunga.

5. Idadi ndogo ya wachezaji kuingia eneo la mpinzani. Yanga wanaposhambulia huwa wanakuwa wachache eneo la mpinzani na hivyo kuwarahisishia wapinzani kuokoa mipira kwa urahisi au krosi nyingi kukosa mtu wa kumalizia.

Mimi haya ndo niliyoyaona,karibuni tuendelee kuwapa ushauri.
 
Sikio la kufa hao walisajili wakina kisinda ili amkomeshe onyango matokeo yake
Msuli wa kimataifa unachanika
 
Pia wahakikishe wanajitahidi kukaza meno kama wanavyokaza mechi za Simba.

Kwa lugha rahisi wachukue vinyago wavivishe jezi za Simba wahisi wako wanapambana na Simba , hapo Club Africain hatatoka hakika

Nje ya hayo basi byebye
Prince Dube akisoma hiki ulicho kiandika hapa, atabakia tu kujisemea kwamba "yule mwenyekiti wenu wa zamani alikuwa sahihi kabisa kuwaita lile jina"
 
Malengo ya yanga na azam ni kuifunga simba.

Ktk hilo wameshafanikiwa ila huko kimataifa hawana tofauti na mwenge unaoangaza vijijini tu na kamwe hata burundi mipakani hauwezi fika.
 
Prince Dube akisoma hiki ulicho kiandika hapa, atabakia tu kujisemea kwamba "yule mwenyekiti wenu wa zamani alikuwa sahihi kabisa kuwaita lile jina"
We Dube hakukufunga kweli
 
Hao warabu hawana mapungufu?
 
Mnaambiwa ukweli lakini mnalete habari za vibonde wenzenu Azam
Kesho mtageuka ngoma mnayosemega
 
Mnaambiwa ukweli lakini mnaleta habari za vibonde wenzenu Azam
Kesho mtageuka ngoma mnayosemega
 
We Dube hakukufunga kweli
Unataka kuleta story za mwaka gani! Mimi naongelea wiki iliyopita!

Kwanza Yanga haiwezi kujifunza kwa timu ambayo anaifunga tu vile apendavyo! Timu gani Ikijitahidi sana, basi inatoa sare!!
 
Hakika aliewaita utopolo aliwaza mbali sana
Unataka kuleta story za mwaka gani! Mimi naongelea wiki iliyopita!

Kwanza Yanga haiwezi kujifunza kwa timu ambayo anaifunga tu vile apendavyo! Timu gani Ikijitahidi sana, basi inatoa sare!!
 
Mnaambiwa ukweli lakini mnalete habari za vibonde wenzenu Azam
Kesho mtageuka ngoma mnayosemega
We umejuaje kama ni ukweli?
Na una uhakika gani kama hawajayafanyia kazi?
 
Hakuna kitu kinauzi kama unahitaji magoli halafu una shambulia kwa taratibu, back pass nyingi, namba ya wachezaji wako ni ndogo kwenye kumi na nane ya mpinzani kulinganisha na washambuliaji wako. Hapo goli utapata vipi?

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Wasiliana na dube kwanza,mpumelelo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…