Yanga chupuchupu kwa Majimaji mjini Songea, zatoshana nguvu

Yanga chupuchupu kwa Majimaji mjini Songea, zatoshana nguvu

Modibo

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
425
Reaction score
700
Mwenye update karibu hapa
----------

Mshambuliaji Donald Ngoma ameifichia aibu timu yake ya Yanga baada ya kusawazisha bao dakika za majeruhi ugenini dhidi ya Majimaji katika mchezo wa ligi uliopigwa kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.


Ngoma alifunga bao hilo dakika ya 79 kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliochongwa na Obrey Chirwa upande wa kulia huku ukimuacha mlango Andrew Ntalla asiwe na la kufanya.


Wenyeji Majimaji walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Peter Mapunda dakika ya 54 baada ya kupokea pasi ya Marcel Boniventure aliyoipitisha katikati ya walinzi wa Yanga.


Yanga wameambulia alama nne katika mechi mbili za nyanda za juu Kusini kufuatia sare ya leo na ushindi wa bao moja walioupata dhidi ya Njombe Mji wikiendi iliyopita.


Winga wa Yanga Emmanuel Martin alishindwa kuendelea na mchezo muda mfupi baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Geofrey Mwashiuya kipindi cha pili baada ya kugongwa na mchezaji wa Majimaji wakati mechi hiyo ikielekea ukingoni.


Yanga wanarejea jijini Dar es Salaam wakiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi tatu wakishinda moja na kupata sare michezo miwili.

CHANZO: Yetu
 
Yanga lazima wapigwe magic water
 
Oya leteni serious updates wengine tuko shimoni muda Huu..
 
majimaji 1-0 yanga
mtibwa 1-1 mbao
ndanda 0-0 prison
lipuli 0-0 ruvu
singida 1-0 stand
MECHI ZINAENDELEA...
 
Back
Top Bottom