Yanga chupuchupu kwa Majimaji mjini Songea, zatoshana nguvu

Kwa mwendo huu, tutatoboa kweli Kimataifa?

Cdhani kama ni sahihi kumlaumu yeyote kwa mpira utaochezwa kwenye viwanja vya Njombe Mji na Majimaji. Timu nzuri hutegemea kiwanja tambarare (plane), chenye nyasi zilizotandawaa na kilicho laini (soft) ili timu inayotandaza soka ardhini ifanye hivyo bila kuathiriwa na uwanja, inayocheza kwa mashambulizi ya kujibiza (counter-attack) imudu kufanya hivyo kwa kasi iitakayo bila ya kuziwiliwa na mabondemabonde ya uwanja, inayocheza mpira wa kutumia nguvu isiangushwe na ugumu ama mabondemabonde ya kiwanja na inayocheza mipira mirefu ama ya juu isiathirike kwa wachezaji wake kuhofia kuumia wanapofika chini baada ya kuwania mipira ya juu. Viwanja vya Majimaji na Njombe vina kasoro zote hizo. Kumbuka hata Cannavaro alitangulia kuelezea ugumu wa mechi ya Majimaji kutokana na hali ya kiwanja hata kabla ya siku ya mechi. Kumbuka Kamusoko ameumia nyonga kutokana na ugumu wa kiwanja cha Njombe. Kumbuka hata ikiwa na Pluijm Yanga iliambulia sare mara kadhaa kiwanjani hapo. Kumbuka hata ikiwa na Pluijm Yanga haikufanya vizuri kwenye kiwanja chengine chenye hali kama hiyo cha Ndanda. Angalau wenyeji wa viwanja hivyo wana ka-natija (advantage) kadogo ka kuwa wameshavizowea. Lakini kwa timu zilizo kwenye daraja moja, ushindi kwenye viwanja kama hivyo unategemea bahati zaidi kuliko uwezo. Na huenda ndio kichocheo kimojawapo cha rushwa kutumika ili timu ijihakikishie ushindi inapokuwa kwenye viwanja kama hivi.
 
vipi kuhusu kutoa sare na lipuli pale uwanja wa Uhuru mkuu?
nadhani tatizo lilikuwa uwanja pia
 
vipi kuhusu kutoa sare na lipuli pale uwanja wa Uhuru mkuu?
nadhani tatizo lilikuwa uwanja pia
Sare ya Lipuli haikuwa mada ya mwanzisha uzi huu, mada yake ni sare ya kiwango cha Yanga kwa mechi ya Majimaji. Sina tatizo na kukupa maoni yangu kuhusu mechi uliyoitaja, ila nawe itabidi uanzishe uzi kuhusu hilo kama huyu wa Majimaji alivyoanzisha. Vinginevyo utaishia kupata mawazo yangu tu ambayo kwa mwelekeo wa swala lako hayatakusaidia sana.
 
Kihistoria yanga hana unavu wa kuwafunga wana lizombe ndani ya Majimaji Ground
 
vipi kuhusu kutoa sare na lipuli pale uwanja wa Uhuru mkuu?
nadhani tatizo lilikuwa uwanja pia
Ndala fc ilitakiwa wapigwe kabisa na mashujaa wa majimaji ili iwe onyo kwao.
Shadrack Nsajigwa anataka uwanja ufungiwe kumbe ni mpuuzi sana yule.
 
unafuatilia ligi kweli we au ngonjera tu..yanga msimu uloisha kashinda majimaji stadium goli moja bila..goli na deus kaseke pasi ya niyo ata timu yako yenyewe huifwatili.yanga ni mbovu t msimu huu usilete sababu sababu zisiso na kichwa wala miguu
 
unafuatilia ligi kweli we au ngonjera tu..yanga msimu uloisha kashinda majimaji stadium goli moja bila..goli na deus kaseke pasi ya niyo ata timu yako yenyewe huifwatili.yanga ni mbovu t msimu huu usilete sababu sababu zisiso na kichwa wala miguu
Angalau msimu mmoja ni mrefu kukumbuka matokeo ya Ligi, lakini wewe unashindwa hata kufuatilia maelezo hayo hayo uliyokurupuka kuyajibu, aibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…