Yanga hali si shwari hata kidogo

Muongezeeni tena kanjibhai mwaka mmoja ili tuendelee kujipigia.
 
Fikra mfu na tena zisizo na maono,mpira hauendeshwi kwa nadharia za kijinga kama hivyo,mambo ya huyu katoka Simba kaja Yanga ndio maana tunafungwa,ni mambo ya kijinga na ya kizamani sana,mpira siku hizi ni science na ni ajira pia,hata wachezaji wanajua hiyo ni ajira yao,haya mambo ya kuanza kuita wachezaji makapi ya Simba ni kuwavunja morali na kuwaharibu zaidi kisaikolojia!Yanga wanatakiwa kuwa kitu kimoja,kurekebisha kasoro ndogo ndogo na kusonga mbele,sio ujinga na matatizo yaanze eti sababu tumefungwa na Simba wakati tuna team nzuri,league tunaongoza na bado tupo mashindano ya kimataifa,mpira hautazamwi kwa mechi moja tu ya Simba na Yanga,lazima tubadilike Watanzania,tisiwe wajinga kila siku,tujifunze kwa wenzetu
 

Yanga ina timu nzuri hata cmba wanalijua hilo,kinachofanyika ss ni kutaka kuwavuruga wachezaji kisaikolojia na hawa jamaa wa cmba km huyu aliyeanzisha huu uzi
 
Hivi Yanga imeanza kufungwa na Simba kipindi cha uongozi wa Manji tu na je baada ya kusajili wachezaji toka Simba. Naomba jibu toka kwako mleta mada?
 
watani tulieni mjenge timu kufunga au kufungwa ni matokeo ya mchezo! Tumewafunga kwasababu za kiufundi kitu ambacho mtu yeyote anaejua soka aliona madhaifu ya yanga na simba pia.

Kufukuza wachezaji wala sio suluhisho! Kaeni mjenge timu asiyekubali kushindwa si mshindani.

Yanga watani zangu hakuna mtu nje ya yanga anaewahujumu, kikulacho kinguoni mwako! Mnakulana wenyewe, kuna watu wanamaslahi binafsi huwa wanacheza na saikolojia yenu! Mechi ya simba na yanga inabidi muwe mmejiandaa kisaikolojia la sivyo mtafukuzana na mwisho wa siku mtabaki na wachezaji wawili.

Kama shabiki wa simba nilifurahi kuwafungeni lakini jinsi mlivyoyapokea matokeo inaonesha ni jinsi gani ambavyo hamjakomaa kisoka!

YANGA KUMBUKENI MANENO HAYA 'MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE'

mungu ibariki tanzania, mungu ibariki SIMBA SPORTS CLUB!
 
Nafukua makaburi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…