Yanga hatarini kufungiwa usajili, Eymael asema asilaumiwe

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara na Kombe la ASFC, Yanga wanaweza kukumbana na rungu la kufungiwa kusajili katika madirisha matatu ya usajili ikiwa ni pamoja na kuondolewa msimu ujao kwenye michuano ya Kimataifa.

Uamuzi huo unaweza kufanywa muda wowote, kutokana na Yanga kushindwa kulipa kwa wakati deni la aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Luc Eymael.

Eymael aliiburuza Yanga kwa Shirikisho la Kimataifa la Soka Duniani (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake miezi michache baada ya kibarua chake kuota nyasi, Septemba 2021.

Hata hivyo miamba hiyo ya soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki ilikubali kumlipa kocha huyo kwa awamu.

Kwa mujibu wa notisi ya malipo ya Eymael, Yanga ilipaswa kumalizana naye ndani ya siku 45 huku kuanzia Juni 9 mwaka huu wakitakiwa kulipa na riba ya asilimia tano hadi juzi Ijumaa ambapo ilikuwa siku ya mwisho kumaliza deni la Dola 66,000 ambazo ni zaidi ya Sh. 157milioni.

Kocha huyo, ameliambia Mwanaspoti kuwa asilaumiwe kwa kile ambacho FIFA inaweza kufanya kufuatia Yanga kushindwa kukamilisha kile ambacho walikubaliana kuhusu malipo yake kwani hadi siku ya mwisho, juzi walikuwa wamemlipa nusu ya kiwango ambacho alitakiwa kupata.

"Nimekuwa nikifanya nao mawasiliano lakini naona wamekuwa kimya, kwa kuwa hili suala limefika kwenye mamlaka husika kwa hiyo tutaona kile ambacho wataamua, wanaweza pia kuingia kwenye adhabu ya kupokonywa pointi tisa,"

"Mwaka 2018 au 2017, Amazulu walikuwa na kesi kama hii, hawakulipa hivyo FIFA iliwalazimisha kulipa au kushuka daraja kabla ya msimu mpya kuanza, siku zote hakuna aliye juu ya sheria," alisema kocha huyo.

Kwa mujibu wa Eymael inamaana kuwa hadi siku ya mwisho ya malipo yote kufanywa, Yanga ilikuwa imemlipa Dola 33,000 (Sh78.8 milioni).

Yanga inaweza kuwa kwenye wakati mgumu zaidi kama FIFA itachukua maamuzi hayo kutokana na baadhi ya wachezaji wao muhimu kuwa mbioni kutimka akiwemo Fiston Mayele anayehusishwa na klabu mbalimbali kubwa ndani na nje ya Afrika kufuatia kuwa mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alitafutwa jana ili kutoa ufafanuzi wa jambo hilo, lakini simu yake haikupokelewa sawa na ilivyokuwa kwa Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo.

Chanzo: Mwanaspoti

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Sasa wataporwaje pointi 9 kwenye ligi ambayo imeisha na wao ndio mabingwa?

Ila Yanga imeandamwa na madeni.

Huku Yanga Princess wanadai, huku Bangala na Djuma Shabani nao wanadai.

Hawajakaa vizuri naye Lucy Eymael naye anawadai.

Nawashauri Yanga wakakope kausha damu walipe madeni yao
 
Mkija kustuka yanga bingwa mpaka 2030.
 
Sawa kumbe kimataifa watacheza ligi y Tanzania
 
Mkija kustuka yanga bingwa mpaka 2030.
Thubutu kwa timu gani?

Maana yule kiungo wenu mliyekuwa mnamtegemea kwa mbio ndio huyo anapaki mabegi.

Djuma Shabani na Bangala nao kama sio kesho basi kesho kutwa tutaskika "senkyu"

Lomalisa naye yupo kwenye tetesi za kwenda Azam

Mitso mliyetudanganya katimkia uarabuni

Mayele naye tumesikia aliripotiwa na vyombo vya nje kuwa kuna watu wanamfata.

Ambaye mna uhakika wa kubaki naye kwa asilimia 60 ni Diarra. Ambaye ni useless bila hao wengine.

Tungeweza kusema mtapata ubingwa kwa kuhonga sasa mixer na madeni mliyokuwa nayo mtaweza ku handle bajeti?
 
Fanya kazi kwa bidii, kunywa maji, tafuta mda wa kupumzika.
 
Ila UTO kama VIKOBA kila kona madeni [emoji205][emoji205][emoji205]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa hao kausa damu ndo balaa zaidi ya hawa wenginee.
 
Hili ndo linaniuma zaidi,

Nyani tuitwe sisi halafu na fedha tulipe sie[emoji24][emoji24][emoji24]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ko ni vawulensiiiiii??
 
Ila Yanga si wamepata pesa mingi ya CAFCC second runner? Kwann wasi clear madeni yote, ili waanze upya kwa amani.

Sasa 157M Nazo wanashindwa kulipaa?? Mmmh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…