Yanga hii itafika mbali

BETONY

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
188
Reaction score
170
Kwanza nianze kwa kusema kuwa mimi ni shabiki kindakindaki wa Yanga, japo miaka miwili iliyopita nilijipa likizo ya kutoifuatilia. Hili la kutoifatilia ilitokana na timu yangu hii kuwa na mambo mengi ya kuudhi, japo ilipokuwa yafanya vibaya, niliumia.

Msimu huu mpya ulianza kwa tambo nyingi sana. Wakati wa usajili nilikaa kimya kuona hii pendwa itawaleta nani. Wengi waliokiwa wanasajiliwa niliwapa tahadhari, kwani najua mpira wa Tanzania una mengi. Lakini baada ya mechi ya leo niwe muwazi na kuiweka furaha yangu hadharani.

Hakika waliofanya usajili safari hii wametuletea watu kweli kweli. Kuanza kwa Zawadi Mauya, mpaka kule mbele hakika kazi hii ilifanyika kwa kuzingatia Yanga inataka nini kwani mpaka benchi la akiba wamekaa wanaume kweli kweli. Niwaambie mashabiki na wapenzi wa Yanga, timu hii tunatakiwa tuipe muda, itafanya makubwa sana, hasa mwalimu atakapowaelewa wachezaji wake. Pia naomba viongozi watulie, wasiwe na maneno mengi kuingilia benchi la ufundi. Yanga hii naitabiria makubwa sana.

Daima mbele, nyuma mwiko.
Asante timu nzima iliyofanya usajili yanga
Wasalaaam
 
Kwa hiyo muda utakuwa unawasubiria tu wajuane sio?
 
Senzo senta half halafu kingwala striker duh utopolo bana
 

Mtafikaje mbali wakati mmesajiliwa wachezaji halafu mishahara inabidi mtafute nyie! Watawakimbia wote na tutaanza na Tusinde
 
Wakati mnasubiri muunganiko,kipigo toka kwa mnyama hadi mtafukuza wachezaji wenu wote tena.

Hata leo kuna wana utopolo wenzio wanasema baadhi ya wachezaji wameuza mechi
 
Demu akikwambia"nioe au tuishi wote"unamwambia ngoja kwanza tuzoeane,mkija kuzoeana tyr ushampa na mimba anakuona mizinguo anaanza kudanga.

Yanga mpaka mkija kuzoena mtakuwa mshavuliwa pichu na Simba na mimba juu,kila timu mtakayokutana nayo mnavuliwa pichu mnapigwa cha kuchutama cha fastafasta.
 
Vyuraaa vimeanzia vilipo ishia ,,,jez zile zile matokeo Yale yale
 
Matokeo na prison yakoje? Hahaha
 
Kama umeangalia mpira wa Yanga vs Prison, hakika moyo mwako utakuwa unakubaliana nami kwamba Yanga inarudi.
 
Hiyo ni kauli yako. Lakini kwa mpira uliopigwa jana, Simba vs Ihefu na Yanga Vs Prison, utakubaliana nami kuwa Yanga imeonesha kuwa nzuri zaidi. Timu yote karibia ni mpya lakini imepiga mpira mkubwa kabisa
 
Wakati mnasubiri muunganiko,kipigo toka kwa mnyama hadi mtafukuza wachezaji wenu wote tena.

Hata leo kuna wana utopolo wenzio wanasema baadhi ya wachezaji wameuza mechi
Hao hawajui maana ya mchezo wa mpira wa miguu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…