Yanga hii ni kama maji usipoyanywa utayaoga, mechi 6 magoli 13 karuhusu magoli 4 tu!

Yanga hii ni kama maji usipoyanywa utayaoga, mechi 6 magoli 13 karuhusu magoli 4 tu!

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Ukiichukia hii timu Awana habari na wewe,,na Wala sio shida zao itakulazimu uukubali ukweli tu maana Amna namna yoyote Ile utaitumia kujifariji, Wao wanachokifanya ni kuacha miguu yao iongee na sio mipasho na propaganda! Kamchapa Ts Galax ya Africa kusini 1-0, kamchapa kaizer chief 4-0, kamchapa Red Arrows 2-1,,kamchapa Simba 1-0,,kamchapa Azam 4-1, na kapoteza moja dhidi ya Augsburg ya ujerumani!

Yanga kwa sasa mpira wanaocheza ni mpira wa klabu bingwa, mbinu na mambo mengi ya kiufundi wamejifunza kwenye ushiriki wao klabu bingwa na kukutana na timu ngumu na tishio barani Africa vimewajenga sana!

Gamond anakabiliana na wewe jinsi unavyokuja ndivyo anavyokupokea! Mechi ya Leo imeonyesha timu iliyokomaa na timu ambayo aijakomaa, Azam walipopata goli waliona wamemaliza kazi na waliona wameiweza yanga wakaamua kupishana na yanga kitendo ambacho ilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo lilikuja kuwagharimu!

Soma Pia: Full Time: Azam FC 1- 4 Yanga SC | Community Shield | Final | Benjamin Mkapa Stadium | 11/08/2024

Gamond uwa anafurahia sana timu ya kupishana nayo na sio ya kupaki bus, unapotaka kupishana na yanga inatakiwa timu yako iwe imekamilika aswaa Kila idara!

N;B Feisal aambiwe aache utoto atakuwa anawagharimu wenzake, kafungua kigoli kaenda kuwakatia mauno mashabiki wa yanga, kilichofata akawasimulie waliomtuma!
 
Hii kasi ya kuisifia yanga kila kukikucha ina mwisho wake...mbaya zaid kinatokea kitimu kidogo hakina hata jina kitaiburagaza mpaka mtalia kama kima
 
Back
Top Bottom