Yanga imechemka kumsajili tena Mrisho Ngasa

Status
Not open for further replies.

AbaMukulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
2,053
Reaction score
3,586
Leo timu ya Yanga imethibitisha kumsajili tena Mrisho Ngassa akitokea Ndanda Fc.

Yanga kwenye hili wamechemka kwani muda umeshamtupa mkono 'Anko Ngassa'

"Mtoto yatima hadeki"

UPDATES:

Uongozi wa klabu ya Yanga umekanusha taarifa zilizoenea mitandaoni zikidai kuwa wameanza mazungumzo na mchezaji wake wa zamani, Mrisho Khalfan Ngassa, ili kumrejesha.

Mkuu wa Kamati ya Kamati ya Usajili na Maadili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, ameeleza kuwa hakuna ukweli juu ya hilo na badala yake mchezaji huyo aliwasili katika makao makuu ya klabu hiyo kusalimia.

Nyika ameeleza kuwa Ngassa aliwasili kuwapa salaam na si kusajiliwa kama ambavyo taarifa nyingi zimekuwa zikieleza.

Ngassa ambaye aliwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio makubwa katika ligi, alijiunga na Mbeya City FC kisha kutimkia Ndanda FC ya Mtwara iliyoepuka kushuka daraja mwishoni mwa msimu.

Wakati huo Yanga kesho inaondoka kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup itakayoanza Juni 3 2018 jijini Nairobi.
 
Nasikia akina nsajigwa, Ally mayay, sekilojo chambua, Peter manyika senior pia wamepewa wito wakurudi nyumbani, wasajili tenaaaaa!


Maaskini ya Mungu Hawa vyura wanatia huruma aiseee!

Hii itakuwa timu au bands of elders??
 
Nasikia akina nsajigwa, Ally mayay, sekilojo chambua, Peter manyika senior pia wamepewa wito wakurudi nyumbani, wasajili tenaaaaa!


Maaskini ya Mungu Hawa vyura wanatia huruma aiseee!

Hii itakuwa timu au bands of elders??
Itabidi watafute bonanza la maveterani wawe wanashiriki
 
Wazee wa "misumari" wanarejea bado tegeta
 
Nakumbuka kipind simba wanasajir watu walisema wanachukua wahenga, lakini wanaweza wakawasaidia hawa wahenga
 
Viongozi wa hizi timu zetu akili zao zimekaa kimende mende sana sijui walizaliwa vyooni! Ndo maana timu zinakuwa masikini miaka zaidi ya 50!! Am fed up na haya matimu yetu!! Africa!!!!!!!
 
Kama huna taarifa nyoso pia anatua yanga

Mpelekee salam bocco, bwana wake ametua yanga
 
Nikukumbushe Ferguson alimsajili Michael Owen akitokea Madrid wakati kaonekana kachoka kwahiyo mpe nafasi ngasa aonyeshe alichonacho baadae utamjaji km anafaa au hafai.
 
Leo timu ya Yanga imethibitisha kumsajili tena Mrisho Ngassa akitokea Ndanda Fc.

Yanga kwenye hili wamechemka kwani muda umeshamtupa mkono 'Anko Ngassa'

"Mtoto yatima hadeki"

Halafu tukisema humu kuwa Yanga wengi huwa wanamatatizo ya akili mnakimbilia Kukasirika, Kununa na hata Kutukana.
 
Tatizo sio viongozi tatizo wachezaji vijana wameshindwa ku prove ubora wao ,bora hao wazee wana msaada kwa timu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…