Yanga ina shida kubwa upande wa kushoto na eneo viungo

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Yanga walifanya kosa kubwa kumwacha Gadiel ,na wakafanya kosa lingine la usajili mbovu wa beki wa kushoto.

Sonzo anamapungufu mengi sn kutokana na sifa anazotakiwa kuwa nazo beki wa pembeni kwa mpira wa kisasa anatakiwa awe na mbio,mwenye uwezo kupanda na kushuka,anaweza kupiga chenga, kumiliki mpira na kupiga cross.

Sonzo hana sifa hata moja kati ya hizo.Hajiamini na akipata mpira ni kubutua mbele bila hata kuangalia anampa nani.

Rollers walipogundua madhaifu yake walikuwa wanapitia kushoto na kuwafanya kina Yondani kupata wakati mgumu sana.Waliotazama mechi ya leo nazani mmeona.

Pia eneo la kiungo Shishimbi anajichanganya sana.

Hajui ni muda gani apandishe mashambulizi na muda gani arudi kukaba chini.

Hali inayopelekea eneo la katika kubaki na mwanya.

Pia viongo hawawezi kipiga pasi ni kubutuabutua tu.

Hakuna utulivu kabsa. Wakikutana na timu zinazozijielewa watapigwa nyingi sn.
 
Sawa umeleweka...ila nauliza Man United tatizo liko wapi?? Simba tatizo liko wapi?? Barca tatizo liko wapi? Azam tatizo liko wapi? Bayern Munich tatizo liko wapi?

Gadiel hakuachwa, alikata mawasiliano na Yanga na hata kuzima simu. Gadiel alishawishiwa aende Simba wakati alipokuwa Yanga.

Yaani alikuwa anaccheza mechi za Yanga huku tayari akijua kuwa atakwenda Simba, haya ndiyo yaliyo nyuma ya pazia na inawezekana kabisa wako wanaSiba walikuwa wanamlipa chochote akiwa bado Yanga.

Gadiel alipendezwa na 'This is Simba' We are Simba back to back...miaka kumi mfululizo ubingwa
 
Pumbavu sana wewe tuache na timu yetu. Kwahyo ulitaka tumbebe kwa nguvu Gadiel? Acha akae simba asugue benchi mpaka akili imkae.
 
....Gadiel alipendezwa na 'This is Simba'...We are Simba...back to back...miaka kumi mfululizo ubingwa.......... ......
😂😂😂 hii Kali 🤣🤣🤣
 
Ulichoandika ni sahihi, Ally Sonso kimsingi si beki wa kushoto Bali ni beki wa kati. Mwalimu aliamua kumchezesha beki ya kushoto baada yule Marcelo Mualami kuonekana kuwa mzito, kama uliangalia mechi ya kwanza, utangundua hata like goli walilotufunga chanzo ni yeye. Hata ile game na K.sharks tatizo alikuwa ni yeye. Hivyo kwangu Mimi Sonso ni zaidi ya yule Mualami Marcelo hasa linapokuja suala LA marking na kukaba. Hata tatizo lipo si uongo, dirisha dogo tunatakiwa kuingia sokoni maalum kwa beki 3. Viungo wako vizuri siyo kama ulivyoelezea mkuu.
 
Wewe ni mwanayanga na unaujua mpira Sonso hakusajiliwa kuwa beki wa pembeni unyumbulifu wake na umakini ndio umepelekea kuwekwa pale. Marcelo kwa mechi za kimataifa/mechi za timu zinazotumia nguvu nyingi bado sana.
Kuhusu Gadiel wala tusiwalaumu viongozi maana jitihada zao ziligonga mwamba.
Pengine kocha amjaribu Mohammed Jaffary labda atatusaidia huku mbeleni ila kwa kipindi hiki cha mpito wacha sonso aendelee anajtuma sana.
 
Sonso ni beki wa kati,halafu hakuna timu iliyokamilika Simba ina tatizo la beki,kwa kifupi hakuna timu isiyo na tatizo.
 
Sonso ni beki wa kati, amepelekwa pembeni kwa hitajio la mchezo, Akiendelea kucheza iyo nafasi ataimudu kwakua mtu wa kazkaz. Papii kinachomfanya asogee ni kuongeza mashambuliz kwakua bado idara ya ushambuliaji haina muunganiko.

kwatimu ilivyo ilo si tatizo mbele kuki kaa sawa hutomuona Papii akisogea kule.
Kinacho fanyika Yondani anasogea na kuziba shimo la papii akiwa amepanda na Sonso anaziba shimo la Yondani.
Kwa ujumla ukuta wa yanga utakua imara kuliko msimu ulio pita.
 
Pamoja na yote ile winga ya rolers iliyokuwa inakabana na sonzo ilikuwa ‘teleza’na sumbufu kweli kweli ndipo mashambulizi yote ya ma- rollers yalikuwa yanaanzia pale
 
Tatizo la Marcelo akipanda anachelewa kurudi lakini si mbaya sana
Ulichoandika ni sahihi, Ally Sonso kimsingi si beki wa kushoto Bali ni beki wa kati. Mwalimu aliamua kumchezesha beki ya kushoto baada yule Marcelo Mualami kuonekana kuwa mzito, kama uliangalia mechi ya kwanza, utangundua hata like goli walilotufunga chanzo ni yeye. Hata ile game na K.sharks tatizo alikuwa ni yeye. Hivyo kwangu Mimi Sonso ni zaidi ya yule Mualami Marcelo hasa linapokuja suala LA marking na kukaba. Hata tatizo lipo si uongo, dirisha dogo tunatakiwa kuingia sokoni maalum kwa beki 3. Viungo wako vizuri siyo kama ulivyoelezea mkuu.
 
Kuhusu Beki 3 uko sahihi Mkuu ingawa kama walivyoeleza wengi Ally Sonso si beki wa kushoto Bali ni beki 4 au 5. Alichezeshwa jana ili kuziba madhaifu ya Mharami.

Hata hivyo kipindi cha kwanza alijitahidi sana ila baadae alichoka kutokana na kutozoea kucheza bamba hiyo. Kwa upende wa viungo hujamtendea haki Papy Kabamba amebadilika sana ndiye ambaye alikuwa key player.

Tatizo lilijitokeza pale Kocha Zahera alipomtoa Mo Banka na Mapinduzi Balama ndiio Town Rollers walipopata nafasi ya kumiliki mpira.

Ila kwa jana Yanga walicheza kwa malengo. Kinachotakiwa kwenye dirisha dogo Yanga wasajili beki 3 halisi na forward mwenye accuracy zaidi.
 
Yeah kweli kabisa,Ally mtoni bado hajaziba vema kama katili Boxer
 
Wewe ni mwanayanga na unaujua mpira Sonso hakusajiliwa kuwa beki wa pembeni unyumbulifu wake na umakini ndio umepelekea kuwekwa pale. Marcelo kwa mechi za kimataifa/mechi za timu zinazotumia nguvu nyingi bado sana.
Kuhusu Gadiel wala tusiwalaumu viongozi maana jitihada zao ziligonga mwamba.
Pengine kocha amjaribu Mohammed Jaffary labda atatusaidia huku mbeleni ila kwa kipindi hiki cha mpito wacha sonso aendelee anajtuma sana.

Huyo Jaffary Mohamed ulimuona kwenye ile mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania? Goli la pili la Ditram Nchimbi lilipitia kwake. Ufupi tu hana sifa ya kuwa beki maana hawezi kukaba na pia hayupo physic! Kiukweli timu yetu itafute tu beki namba tatu mwenye sifa ya kukaba na kushambulia kwa pamoja. Pengo la Gadiel Michael bado lipo wazi.

Marcelo kwenye kukaba ni 0! na Sonso kwa kweli jana alikuwa ni uchochoro ule upande wake, ingawa ni bora aendelee kuanza yeye kuliko Marcelo.
 
Tatizo kubwa litakapokamilika mbele ya safari haina strikers wafungaji mabao
 
Yanga walifanya kosa kubwa kumwacha Gadiel ,na wakafanya kosa lingine la usajili mbovu wa beki wa kushoto.

Sonzo anamapungufu mengi sn kutokana na sifa anazotakiwa kuwa nazo beki wa pembeni kwa mpira wa kisasa anatakiwa awe na mbio,mwenye uwezo kupanda na kushuka,anaweza kupiga chenga, kumiliki mpira na kupiga cross.

Sonzo hana sifa hata moja kati ya hizo.Hajiamini na akipata mpira ni kubutua mbele bila hata kuangalia anampa nani.

Rollers walipogundua madhaifu yake walikuwa wanapitia kushoto na kuwafanya kina Yondani kupata wakati mgumu sana.Waliotazama mechi ya leo nazani mmeona.

Pia eneo la kiungo Shishimbi anajichanganya sana.

Hajui ni muda gani apandishe mashambulizi na muda gani arudi kukaba chini.

Hali inayopelekea eneo la katika kubaki na mwanya.

Pia viongo hawawezi kipiga pasi ni kubutuabutua tu.

Hakuna utulivu kabsa. Wakikutana na timu zinazozijielewa watapigwa nyingi sn.
Hawana uwezo wa kumiliki mpira kwenye zile dakika chache zilizo baki ilitakiwa wamiliki mpira kwa kupigiana pasi ili kupoteza muda
 
Back
Top Bottom