Yanga inakwenda kutufufundisha jinsi ya kushangilia, basi kama la Liverpool lakodishwa afrika kusini, burudani ni next level, haijawahi kutokea

Yanga inakwenda kutufufundisha jinsi ya kushangilia, basi kama la Liverpool lakodishwa afrika kusini, burudani ni next level, haijawahi kutokea

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
"Yanga tunakwenda kuwafundisha watu jinsi ya kushangilia UBINGWA"

"Tofauti ya Yanga na timu zingine ni kwenye ufanyaji wa shughuli zake, Just imagine kuna watu ubingwa waliubeba kwenye Kenta"

"Tumeomba viongozi wa Uwanja wa Sokoine na wa bodi ya ligi kusogeza nyuma muda wa kucheza kutoka saa 10 Jioni hadi saa 9 alasili ili Wananchi baada ya mechi waanze kuserebuka na kombe lao"

"Kwa kuwathamini mashabiki wetu baada ya kumaliza shangwe uwanjani Sokoine, sherehe zitaendelea, kutakuwa na After part kama kawaida jijini Mbeya"

"Jumapili tutarudi Dar na ndege ✈️ kama kawaida yetu, na tayari Yanga tumeshashusha basi jipya maalumu kwa ajili ya kushangilia Ubingwa wetu wa mara ya (28)"

"Basi letu jipya limeshavuka boda kuja Tanzania,, Basi letu halina tofauti na basi la Liverpool, Real Madrid, Manchester city,, Tarehe 24 Juni litakuwa limeshafika Dar es Salaam"

"Kwa mara ya kwanza Tanzania basi la namna hii linaletwa na Yanga SC. Basi letu jipya ndilo litawabeba Wachezaji wetu terminal (3) Jijini Dar es Salaam, litasindikizwa na farasi, gari maalumu hadi Airport"

"Wananchi wanapaswa kufika mapema terminal (3) siku ya jumapili"

"Tukishatua litawabeba Wachezaji wetu, tutapita kwenye baadhi ya mitaa kama Kamata, Chang'ombe, MSIMBAZI, hadi Jangwani. Na baada ya kufika Jangwani tutafanya DUA maalumu kumshukuru Mungu"

"Baada ya DUA watu wote watapiga mpunga, tutakuwa na chakula kwa ajili ya mashabiki wote pale klabuni Jangwani,, Kisha tutamkabidhi kombe mwenyekiti wetu Dr Mshindo Msolla"

"Nimeshaongea na kamanda wa usalama jijini Dar es Salaam kuomba maaskari kutulinda kwenye msafara wetu,, tutazunguka mitaa yote jijini Dar es Salaam tutaufunga mji ... Tutakwenda hadi Posta zilipo ofisi za GSM kushangilia kombe letu"

"Baada ya kutoka GSM, sherehe zitahamia KIDIMBWI, mashabiki wetu wote watapata fursa ya kupiga picha na kombe"

"Kutakuwa na burudani za kutosha kutoka kwa wasanii wakubwa hapa nchini kama wakina Marioo nk...."

"Kuna msanii mkubwa sana atakuja kutumbuiza kwenye sherehe hizi za Ubingwa wetu. Ni rafiki yangu mkubwa sana na anajua matatizo niliyopitia kwa muda ule"

"Wananchi wanapaswa kujua, hili ni basi letu Wanayanga litakuwepo kushangilia UBINGWA wa (FA) pia, sherehe tutàfanya mwezi mzima wa (7), Wale wawe hoi na sie tue hoi 😆"

🔍 Haji Manara msemaji wa Yanga SC
 
Ushamba na ulimbukeni ni mzigo sana

Kwasababu umenunua chupi ya Gucci kwa $200 umeona kuivaa ndani ya nguo watu hawawezi kujua kuwa nawewe unavaa vitu vya thamani mpaka ukaivaa nje kama superman?
 
"Yanga tunakwenda kuwafundisha watu jinsi ya kushangilia UBINGWA"

"Tofauti ya Yanga na timu zingine ni kwenye ufanyaji wa shughuli zake, Just imagine kuna watu ubingwa waliubeba kwenye Kenta...
Kudadadeq !!! Safari hii lazima tutembee uchi tukiongozwa na morisoni wetu huku msukule wetu ukipiga ngoma. Miaka 4 bila kombe si mchezo!!
 
"Yanga tunakwenda kuwafundisha watu jinsi ya kushangilia UBINGWA"

"Tofauti ya Yanga na timu zingine ni kwenye ufanyaji wa shughuli zake, Just imagine kuna watu ubingwa waliubeba kwenye Kenta...
Huku mnasema basi letu jipya, kichwa cha habari mmekodisha..doh ama kweli Utopolo aisee..
 
Wanastahili miaka minne ni mingi sana kama mlibeba mapinduzi tu mkafanya fujo dar nzima mmeshinda kombe ni haki yenu.
 
Back
Top Bottom