Yanga inapata faida kweli kucheza ligi kuu tu, huku kimataifa hawapo?

Yanga inapata faida kweli kucheza ligi kuu tu, huku kimataifa hawapo?

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Moja kati ya nguzo kuu za mpira wa sasa ni kucheza mashindano ambayo yatakuwa yanaisaidia club kujiendesha pasipo kutegemea sana kupitisha mabakuli kwa matajiri na wadhamini ndio maana ulaya kocha anaweza akafukuzwa sababu ya kutolewa uefa kizembe au kutofuzu kabisa huwa inachukuliwa kama hasara kubwa kwa timu.

Kwa muda mrefu yanga wamefocus sana kwenye makombe ya ndani ambayo hayana pesa wala faida ya maana, ligi kuu ukichukua ubingwa ile pesa wanayolipwa kama zawadi unaweza kuta ni mshahara wa mayele tu wa miezi kadhaa sasa hebu fikiria club nzima itajiendeshaje kwa pesa ile maana ni ndogo sana

Nilitegemea yanga kwa kikosi kile now ingekuwa robo fainal CAF maana naona ligi ya ndani wapo vizuri sana ila CAF kama kuna pepo sijui maana kila yanga ikinusa CAF basi makundi ndio mwisho wao

Ila CAF kuna pesa, simba ilipovuka robo fainali mara kwa mara walikuwa wakipata bilioni 1 na ushee na juzi naskia wamepata milioni 800.

Tukubali ukweli Yanga inahitaji kujiongeza sana kwenye mashindano ya kimataifa maana ligi za ndani mtaishia kuendesha Club kwa majashoo ya wadhamini na masponsa wa Gsm wakati kile kikosi kina uwezo wa kupambana kimataifa na mkachota pesa ndefu ambayo itasaidia kwenye uendeshaji wa Club.

Najua mtakuja kuniita makolo ila timu inatakiwa ibadilike sana maana mnapata wachezaji wazuri lakini hamuwatumii vizuri kimataifa wawaingizie pesa, Mtu kama mayele mnaweza mkawa nae msimu na msimu ujao matajiri wakampandia dau akaondoka na ukiangalia mmemtumia vyema ligi ya ndani tu kimataifa hampo.
 
Last edited:
Wanamfurahisha yule rafiki yake na Makonda...
Ni kama waarabu tu na ligi zao za mafuta Oman...
 
Wametumia kiasi gani kwenye mashindano hayo yaliyowapa 3.8bn?
Nauli, kambi, hotels etc..
Pia wana wafadhili ,mapato ya majengo yao.Hivyo imewasaidia sana kupunguza gharama.
 
Pia wana wafadhili ,mapato ya majengo yao.Hivyo imewasaidia sana kupunguza gharama.
Wametumia kiasi gani kwenye mashindano hayo ya Africa?
Ili tujue kuwa zawadi hazilipi gharama za mashindano au zinalipa na faida juu.
Usikwepe swali.
 
Wametumia kiasi gani kwenye mashindano hayo ya Africa?
Ili tujue kuwa zawadi hazilipi gharama za mashindano au zinalipa na faida juu.
Usikwepe swali.
Sina exact figure lakini kwenye bajeti yao ya mwaka kila unapoingia kwenye hatua nyingine inakuwa ni msaada wa kupunguza matumizi yaliyokusudiwa.

Kuna timu zilishiriki na kuondolewa bila kupata chochote licha ya kuingia gharama. Kuna timu hata ilikosa nauli ya kwenda Libya.
Kipato chochote unachopata extra is a bonus regardless ya matumizi uliyokwishapanga.
Ukiangalia kwa angle ya ushabiki mimi sipo huko.
 
Wametumia kiasi gani kwenye mashindano hayo yaliyowapa 3.8bn?
Nauli, kambi, hotels etc. kalumanzilas, sprays, bribe for supervisors of dressing rooms, cost of purchasing black cats etc
 
Umeuliza swali la msingi mishabiki maandazi ya utopolo inajibu pumba.
 
Yanga ni club inaayoendeshwa kwa hasara 99% maana hawafanyi hata biashara ya kuuza wachezaji huwa hawanunuliwi na club zingine ila huwa wanaondoka bure baada ya mkataba kuisha.

Nafikiri ni watu wachache tu wenye pesa zao wameamua kuifadhili lakin hakuna faida yoyote wanayopata
 
Tangu simba wameanza kucheza kimataifa wamepata mafanikio gani hata makao makuu hawana?
Zaidi tu timu imeuzwa kwa Moo kupitia bango lililo andikwa Tsh. Bilioni 20! Ukiwauliza hiyo Bilioni 20 iko wapi, hata hawajui! Eti sisi muhimu timu ishinde na kuchukua mataji!! 😁😁😁

Mpaka kesho ukiwauliza ofisi ya timu iko wapi na kushiriki kwao kimataifa, hawajui! 🤔Jengo la klabu lenyewe ukifika hata mlango wa kuingilia haujulikani ulipo! Wamachinga wamejaa mpaka madirishani!! 😬😬
 
Back
Top Bottom