Moja kati ya nguzo kuu za mpira wa sasa ni kucheza mashindano ambayo yatakuwa yanaisaidia club kujiendesha pasipo kutegemea sana kupitisha mabakuli kwa matajiri na wadhamini ndio maana ulaya kocha anaweza akafukuzwa sababu ya kutolewa uefa kizembe au kutofuzu kabisa huwa inachukuliwa kama hasara kubwa kwa timu.
Kwa muda mrefu yanga wamefocus sana kwenye makombe ya ndani ambayo hayana pesa wala faida ya maana, ligi kuu ukichukua ubingwa ile pesa wanayolipwa kama zawadi unaweza kuta ni mshahara wa mayele tu wa miezi kadhaa sasa hebu fikiria club nzima itajiendeshaje kwa pesa ile maana ni ndogo sana
Nilitegemea yanga kwa kikosi kile now ingekuwa robo fainal CAF maana naona ligi ya ndani wapo vizuri sana ila CAF kama kuna pepo sijui maana kila yanga ikinusa CAF basi makundi ndio mwisho wao
Ila CAF kuna pesa, simba ilipovuka robo fainali mara kwa mara walikuwa wakipata bilioni 1 na ushee na juzi naskia wamepata milioni 800.
Tukubali ukweli Yanga inahitaji kujiongeza sana kwenye mashindano ya kimataifa maana ligi za ndani mtaishia kuendesha Club kwa majashoo ya wadhamini na masponsa wa Gsm wakati kile kikosi kina uwezo wa kupambana kimataifa na mkachota pesa ndefu ambayo itasaidia kwenye uendeshaji wa Club.
Najua mtakuja kuniita makolo ila timu inatakiwa ibadilike sana maana mnapata wachezaji wazuri lakini hamuwatumii vizuri kimataifa wawaingizie pesa, Mtu kama mayele mnaweza mkawa nae msimu na msimu ujao matajiri wakampandia dau akaondoka na ukiangalia mmemtumia vyema ligi ya ndani tu kimataifa hampo.