aka2030
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 2,657
- 3,679
Hivi karibuni uongozi mpya wa klabu ya Yanga SC chini ya mwenyekiti wake Yusuf Manji uliamua kubadilisha Sekretariati iloyokuwepo baada ya kumaliza muda wake mwezi Novemba 2014, na kutangaza sekretariati mpya chini ya katibu mkuu mpya Dr Jonas Tiboroha, Mkurugenzi wa Fedha Baraka Desdeuth, Mkuu wa Sheria Frank Chacha, Mkuu wa Masoko Omar Kaya na Mkuu wa Idara ya Habari Jerry Muro.
Wanachama wengi walishangazwa na mabadiliko hayo ya ghafla ili hali wafanyakazi waliokuwepo Katibu Mkuu Beno Njovu, Mkurugenzi wa Fedha Denis Oundo, Mkurugenzi wa Masoko George Simba, Afisa Habari Baraka Kizuguto, Mhasibu Rose Msamila na Sekretari Zayana Abdul walikua wakifanya kazi zao vizuri na kwa uweledi mkubwa.
Ila kwa kuwa Yanga ya sasa ni ya mabavu na hakuna mwenye uwezo wa kuhoji juu ya suala lolote kuanzia Kamati ya Utendaji, Wanachama, Baraza la wazee, Mwenyekiti aliyejiongezea muda nje ya katiba ndio amekua na maamuzi yote na kamati yake ya utendaji aliyoiweka haina mamlaka yoyote.
Kutokana na uendeshwaji huo wa mabavu umeipelekea Yanga kuwa na kesi zaidi ya nne FIFA zikisubiria maamuzi, na nyingine katika mahamaka za Tanzania,
Kudhihirisha hilo na kuonyesha Kamati ya Utendaji iliyopo ni hewa, isiyokuwa na maamuzi wal kujitambua kulingana na taaluma zao na nyadhifa mbalimbali walizonazo katika taasisi wanazoziongoza, wamekua ni watu wa ndio katika maamuzi yoyote yanayotolewa yawe mazuri au mbaya kwa maslahi yao na mwenyekiti wao anayewaongoza.
Baadhi yao ni :
Mr Fumbuka - Mkurugenzi wa Core Security
Mohamed Nyegi - Mkurugeni wa Fedha Stanbic Bank
Waziri Barnabas - Mkurugenzi wa Fedha NMB
Seif Ahemd 'Magari' - Mfanyabiashara mkubwa nchini
Isaac Chanji - Afisa Usalma wa Taifa na mwakilishi wa marekani nchini Tanzania kwenye mradi wa Symbion Power
Mosses Katabaro - Kamanda wa CCM Vyuo vikuu nchini na mfanyabiashara mkubwa nchini
Abbas Tarimba - Mkurugenzi wa Bodi ya Bahati Nasibu na mbunge mtarajiwa wa Kinondoni
Clement Sanga - Mhandisi anayejenga miradi mingi ya NHC mjini Dodoma
Sam Mapande - Mwanasheria mkongwe wa CRDB na CCM
Tazama baadhi ya email za maelekezo ya kuwabambikia kesi wafanyakazi hao waliomaliza muda wao kwa lengo la kupoteza na kufunika mabaya yake anayotaka kuyafanya kabla ya kuondoka madarakani kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari kutoka kwa mwanasheria wa klabu ya Yanga Frank Chacha ambaye aliyesaidia kupatikana kwa email hizo kwa lengo la kuwasaidia wana Yanga wainusuru klabu yao isipotelee mikononi mwa mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji.