Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Mshika mawili moja humponyoka na wakati mwingine hukosa vyote.Zahera anataka vyote,vya Yanga na vya timu ya taifa. Yanga wanamechi ngumu na muhimu wiki moja ijayo na huu ndo ulikua muda muafaka wa kocha kuandaa timu yake lakini hayupo ameacha program. Aliacha program wakati yupo Afcon wala haikusaidia chochote amerudia tena kuacha programe mbayo anamuachia kocha wa viungo. Zahera ni mtaalamu wa Saikolojia,anajua sn kucheza na akili za mashabiki ampaka wanamuani hata kwa jambo ambalo haliwezekani. Ukweli ni kwamba Yanga kuna shida kubwa ya msingi. Siioni Yanga ikifurukuta mbele ya Pyramid. Maono Yangu yanaonyesha Yanga ikipigwa nje ndani ushindi wa Mwanza unaweza kuwa sare tasa.