Yanga itafungwa nje ndani.

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Mshika mawili moja humponyoka na wakati mwingine hukosa vyote.Zahera anataka vyote,vya Yanga na vya timu ya taifa. Yanga wanamechi ngumu na muhimu wiki moja ijayo na huu ndo ulikua muda muafaka wa kocha kuandaa timu yake lakini hayupo ameacha program. Aliacha program wakati yupo Afcon wala haikusaidia chochote amerudia tena kuacha programe mbayo anamuachia kocha wa viungo. Zahera ni mtaalamu wa Saikolojia,anajua sn kucheza na akili za mashabiki ampaka wanamuani hata kwa jambo ambalo haliwezekani. Ukweli ni kwamba Yanga kuna shida kubwa ya msingi. Siioni Yanga ikifurukuta mbele ya Pyramid. Maono Yangu yanaonyesha Yanga ikipigwa nje ndani ushindi wa Mwanza unaweza kuwa sare tasa.
 
Nchi jirani wanateseka sana
 
Mkuu relax, kama Simba walitolewa na US Dong ajabu iko wapi Yanga kutolewa na Pyramid? au kocha wa Simba na yeye aliacha program ya mazoezi?
 
Ya Zahera yanakuhusu nini wewe kila siku Zaherazahera?Kambi ya south Africa ilileta matokeo hasi au chanya?

Acha ukilaza mwamba mpira sio uadui kila siku kuzusha mambo ya kifala ksa Yanga na Zahera.Kama una jambo la maana litoe kwa staha kwa kujenga hoja sio vioja na kejeki.Unaweza iponda Yanga sawa.msimu ukaisha mkawa simba ndo mabingwa mkatolewa hatua ya awali tena na Yanga ikasogea mbele tena.
 
Ila ukifanya tathmini ya kina na kuachana na ushabiki; unaona kabisa Mwinyi Zahera hatufikishi kokote. Anyway ngoja tu nijinyamazie ili nisiwakwaze mashabiki wenzangu wanaomkubali huyu kocha.
 
Kuna timu ilikuwa South Africa kwenye preseason wakati Yanga wakisemekana wanakula matikikiti huko Morogoro.
Leo wako wapi hao jamaa zetu. Wanesajili hadi Wahindi wakidhani tunacheza Cricket.
 
Mkuu relax, kama Simba walitolewa na US Dong ajabu iko wapi Yanga kutolewa na Pyramid? au kocha wa Simba na yeye aliacha program ya mazoezi?
Huwa wanaweweseka sana hawa jamaa.

Hata na mie naungana nawe Mkuu ,Yanga hata akitolewa hamna la ajabu kabisaaa. Cha zaidi huu ugonjwa walionao ndio utakuwa umepata dawa.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Msitafute kisingizio, msubiri tu mvua ya magoli. Hata awepo huyo unaemlilia unadhani utafurukuta kwa Pyramid? Kwa mchezaji gani wa maana pale mbele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…